Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Mei 2027 › 10 Mei

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 10 Mei 2027

Jumatatu · Juma la 7 la Pasaka

Sikukuu na watakatifu

Jumatatu ya Juma la 7 la Pasaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: nyeupe

Mt. Yohane wa Avila, padre na mwalimu wa Kanisa · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Mdo 19:1–8

1Ikawa kwamba Apolo alipokuwa Korintho, Paulo akapita nyanda za juu na kufika katika mji wa Efeso, na akakuta wanafunzi kadhaa huko. 2Paulo akawaambia, “Je, mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” Wakamwambia, “Hapana, hatukuweza hata kusikia kuhusu Roho Mtakatifu.” 3Paul alisema, “Sasa ninyi mlibatizwaje?” Wakasema, “Katika ubatizo wa Yohana. 4Basi Paulo akajibu, “Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba. Akawaambia wale watu kwamba wanapaswa kumwamini yule ambaye angekuja baada yake, yaani, Yesu.” 5Watu waliposikia habari hii, wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. 6Na ikawa Paulo alipoweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao na wakaanza kunena kwa lugha na kutabiri. 7Jumla yao walikuwa wanaume wapatao kumi na wawili. 8Paulo alienda katika sinagogi akanena kwa ujasiri kwa muda wa miezi mitatu. Alikuwa akiongoza majadiliano na kuwavuta watu kuhusu mambo yanayohusu ufalme wa Mungu.

Wimbo wa katikati

Zab 68:1–6

1Kwa kiongozi wa muziki; Zaburi ya Daudi, wimbo. Mungu ainuke, maadui zake watawanyike; pia wale wamchukiao wakimbie mbele zake. 2Kama moshi uondoshwavyo, hivyo uwaondoshe wao; kama nta iyeyukavo mbele ya moto, hivyo waovu waangamizwe uweponi mwa Mungu. 3Bali wenye haki wafurahi; washangilie mbele za Mungu; washangilie na kufurahi. 4Mwimbieni Mungu! Lisifuni jina lake! Msifuni yule aendeshaye farasi kwenye tambarare ya bonde la Mto Yordani! Yahwe ni jina lake! Shangilieni mbele zake! 5Baba wa yatima, na mwamuzi wa wajane, ni Mungu anayeishi mahali patakatifu. 6Mungu huwaweka wakiwa katika familia; yeye huwafungua wafungwa kwa kuimba bali waasi huishi katika ardhi kavu.

Injili

Yn 16:29–33

29Wanafunzi wake wakamwambia, “Unaona, sasa unaongea wazi wazi na hautumii mafumbo. 30Sasa, tunajua kwamba unajua mambo yote, na hauhitaji mtu yoyote akuulize maswali. Kwa sababu hii tunaamini kuwa unatoka kwa Mungu. 31Yesu akawajibu, “Sasa mmeamini?” 32Tazama, saa inakuja, ndiyo na hakika imefika, ambapo mtatawanyika kila mmoja na kwa wa kwao mtaniacha mwenyewe. Lakini siko peke yangu kwa sababu Baba yupo nami. 33Nawaambia mambo haya ili kwamba ndani yangu muwe na amani. Duniani mna matatizo, lakini jipeni moyo, nimeushinda ulimwengu.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 10 Mei

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki