Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Mei 2027 › 6 Mei

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 6 Mei 2027

Alhamisi · Juma la 6 la Pasaka

Sikukuu na watakatifu

Kupaa kwa Bwana

Sherehe · Rangi ya liturujia: nyeupe

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Mdo 1:1–11

1Kitabu cha zamani nilikiandika, Theofilo, nikisema yote Yesu aliyoanza kufanya na kufundisha, 2mpaka siku ambayo Yeye alipokelewa juu. Hii ilikuwa baada ya kutoa amri kupitia Roho Mtakatifu kwa mitume aliokuwa amewachagua. 3Baada ya mateso yake, Yeye alionekana kwao akiwa hai pia na vithibitisho vingi vikishuhudia. Kwa siku arobaini alijidhihirisha kwao, na alizungumza kuhusu ufalme wa Mungu. 4Alipokuwa akikutana pamoja nao, aliwaamuru wasiondoke Yerusalemu, lakini wasubiri kwa ajili ya ahadi ya Baba, ambayo, alisema, “Mlisikia kutoka kwangu 5kwamba Yohana alibatiza kabisa kwa maji, lakini mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu katika siku hizi chache.” 6Na walipokuwa wamekutanika pamoja walimuuliza, “Bwana, hivi huu ndio muda utakaowarudishia Israeli ufalme?” 7Yeye akawaambia, “Siyo sawa kwenu kujua wakati au majira ambayo Baba amekusudia kwa mamlaka yake mwenyewe.” 8Lakini mtapokea nguvu, wakati Roho Mtakatifu atakapokuja juu yenu, na ninyi mtakuwa mashahidi wangu kote katika Yerusalemu na Uyahudi yote na Samaria mpaka mwisho wa nchi.” 9Bwana Yesu alipokwisha yasema haya, wakiwa wanatazama juu, Yeye aliinuliwa juu, na wingu likamfunika wasimwone kwa macho yao. 10Wakati wanatazama mbinguni kwa makini akienda, ghafla, watu wawili walisimama katikati yao wamevaa mavazi meupe. 11Walisema, “Enyi watu wa Galilaya, kwa nini mnasimama hapa mkitazama mbinguni?” Huyu Yesu aliyepaa juu mbinguni atarudi kwa namna ile ile kama mlivyomuona akienda mbinguni.

Wimbo wa katikati

Zab 47:1–2, 5–8

1Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya wana wa Korah. Pigeni makofi, enyi watu wote; mpigieni Mungu kelele za ushindi. 2Kwa maana Yahwe Aliye Juu anatisha; ni Mfalme mkuu dunia yote. 5Mungu ameinuliwa juu kwa shangwe, Kwa mbiu ya shangwe Yahwe yu juu. 6Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa; mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa. 7Kwa maana Mungu ni Mfalme duniani kote; mwimbieni mkiwa na uelewa. 8Mungu anatawala mataifa yote; Mungu hukaa kwenye kiti cha enzi.

Somo la pili

Efe 4:1–13

1Kwa hiyo, kama mfungwa kwa ajili ya Bwana, nawasihi mtembee sawasawa na wito ambao Mungu aliwaita. 2Muishi kwa unyenyekevu mkuu na upole na uvumilivu. Mkichukuliana katika upendo. 3Fanyeni bidii kuutunza umoja wa Roho katika kifungo cha amani. 4Kuna mwili mmoja na Roho moja, kama ambavyo pia mlikuwa mmeitwa katika uhakika wa taraja moja la wito wenu. 5Na kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja, 6na Mungu mmoja na Baba wa wote. Yeye yuko juu ya yote, na katika yote na ndani ya yote. 7Kwa kila mmoja wetu amepewa kipawa kulingana na kipimo cha kipawa cha Kristo. 8Ni kama maandiko yasemavyo: “Alipopaa juu sana, aliongoza mateka katika utumwa. Akatoa vipawa kwa watu.” 9Ni nini maana ya, “Alipaa,” isipokuwa kwamba alishuka pia pande za chini za dunia? 10Yeye ambaye alishuka ni mtu yuleyule ambae pia alipaa mbali juu ya mbingu zote. Alifanya hivi ili uwepo wake uwe katika vitu vyote. 11Kristo alitoa vipawa kama hivi: mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji, na waalimu. 12Alifanya hivi kuwawezesha waumini kwa ajili ya kazi ya huduma, kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo. 13Anafanya hivi hadi sisi sote tufikie umoja wa imani na maarifa ya mwana wa Mungu. Anafanya hivi hadi tuweze kukomaa kama wale waliofikia kimo kamili cha Kristo.

Injili

Mk 16:15–20

15Akawaambia, “ Enendeni ulimwenguni mwote, na kuhubiri injili kwa viumbe vyote. 16Yeyote aaminiye na kubatizwa ataokolewa, na yule asiyeamini atahukumiwa. 17Ishara hizi zitaambatana na wote waaminio. Kwa jina langu watatoa pepo. Watasema kwa lugha mpya. 18Watashika nyoka kwa mikono yao, na hata wakinywa kitu chochote cha kufisha hakitawadhuru. Wataweka mikono kwa wagonjwa, nao watakuwa wazima”. 19Baada ya Bwana kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu. 20Wanafunzi wakaondoka na kuhubiri kila mahali, wakati Bwana akifanya kazi nao na kulithibitisha neno kwa miujiza na ishara zikifuatana nao.

Watakatifu wa 6 Mei

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki