Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 8 Aprili

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 8 Aprili 2027

Alhamisi · Juma la 2 la Pasaka

Sikukuu na watakatifu

Alhamisi ya Juma la 2 la Pasaka

Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: nyeupe

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Mdo 5:27–33

27Walipokwisha kuwaleta, waliwaweka mbele ya baraza. Kuhani mkuu aliwahoji 28akisema, “Tuliwaamuru msifundishe kwa jina hili, na bado mmeijaza Yerusalemu kwa fundisho lenu, na kutamani kuleta damu ya mtu huyu juu yetu.” 29Lakini Petro na mitume wakajibu, “Lazima tumtii Mungu kuliko watu. 30Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, mliyemuua, kwa kumtundika juu ya mti. 31Mungu alimtukuza katika mkono wake wa kuume, na kumfanya kuwa Mkuu na mwokozi, kutoa toba kwa Israeli, na msamaha wa dhambi. 32Sisi ni mashahidi wa mambo haya, na Roho Mtakatifu, ambaye Mungu amemtoa kwa wale wanaomtii.” 33Wajumbe wa baraza waliposikia hivi, walishikwa na hasira wakataka kuwaua mitume.

Wimbo wa katikati

Zab 34:1, 8, 16–19

1Zaburi ya Daudi; wakati alipojifanya kuwa mwendawazimu mbele ya Abimeleki, ambaye alimtoa yeye nje. Nitamsifu Yahwe wakati wote, siku zote sifa zake zitakuwa mdomoni mwangu. 8Onjeni muone Yahwe ni mzuri. Amebarikiwa mtu yule ambaye Yahwe ni kimbilio lake. 16Uso wa Yahwe uko kinyume na wale watendao uovu, kuikatilia mbali kumbukumbu yao duniani. 17Wenye haki hulia na Yahwe husikia na kuwaokoa kwenye matatizo yao yote. 18Yahwe yu karibu nao waliovunjika moyo, naye huwaokoa waliogandamizwa rohoni. 19Mateso ya wenye haki ni mengi, bali Yahwe huwaokoa nayo yote.

Injili

Yn 3:31–36

31Yeye atokaye juu, yu juu ya yote. Yeye aliye wa ulimwengu anatoka ulimwenguni na huongea mambo ya ki ulimwengu. Yeye atokaye mbinguni yuko juu ya yote. 32Yeye hushuhudia yale aliyoyaona na kuyasikia, lakini hakuna apokeaye ushuhuda wake. 33Yeye aliye pokea ushuhuda wake amehakikisha kuwa Mungu ni mkweli. 34Kwa sababu yeye aliyetumwa na Mungu huongea maneno ya Mungu. Kwa kuwa hampi Roho kwa kipimo. 35Baba humpenda Mwana na amempa vitu vyote mikononi mwake. 36Yeye amwaminiye Mwana anao uzima wa milele, lakini kwa yeye asiye mtii Mwana hatauona uzima, bali ghadhabu ya Mungu hushikamana juu yake.

Watakatifu wa 8 Aprili

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki