Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 7 Aprili

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 7 Aprili 2027

Jumatano · Juma la 2 la Pasaka

Sikukuu na watakatifu

Jumatano ya Juma la 2 la Pasaka

Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe

Mt. Yohane Baptista de la Salle, padre · Kumbukumbu

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Mdo 5:17–26

17Lakini kuhani mkuu aliinuka, na wote waliokuwa pamoja naye (ambao ni wa dhehebu la masadukayo); na walijawa na wivu 18wakanyosha mikono yao kuwakamata mitume na kuwaweka ndani ya gereza la jumla. 19Na wakati wa usiku malaika wa Bwana akaifungua milango ya gereza na kuwaongoza nje na kusema, 20“Nendeni, mkasimame hekaluni na kuwaambia watu maneno yote ya Uzima huu.” 21Waliposikia hili, waliingia hekaluni wakati wa kupambazuka na kufundisha. Lakini, kuhani mkuu alikuja na wote waliokuwa naye, na kuitisha baraza lote kwa pamoja, na wazee wote wa watu wa Israeli, na kuwatuma gerezani ili kuwaleta mitume. 22Lakini watumishi waliokwenda, hawakuwakuta gerezani, walirudi na kutoa taarifa, 23“Tumekuta gereza limefungwa vizuri salama, na walinzi wamesimama langoni, lakini tulipokuwa tukifungua, hatukuona mtu ndani.” 24Sasa wakati jemedari wa hekalu na makuhani wakuu waliposikia maneno haya, waliingiwa na shaka kubwa kwa ajili yao wakiwaza litakuwaje jambo hili. 25Kisha mmoja akaja na kuwaambia, “Watu mliowaweka gerezani wamesimama hekaluni na wanafundisha watu.” 26Hivyo jemedari alienda pamoja na watumishi, na wakawaleta, lakini bila ya kufanya vurugu, kwa sababu waliwaogopa watu wangeweza kuwapiga kwa mawe.

Wimbo wa katikati

Zab 34:1–8

1Zaburi ya Daudi; wakati alipojifanya kuwa mwendawazimu mbele ya Abimeleki, ambaye alimtoa yeye nje. Nitamsifu Yahwe wakati wote, siku zote sifa zake zitakuwa mdomoni mwangu. 2Nitamsifu Yahwe! walio onewa wasikie na kufurahi. 3Msifuni Yahwe pamoja nami, kwa pamoja tuliinue jina lake. 4Nilimuomba Yahwe msaada naye akanijibu, akanipa ushindi juu ya hofu yangu yote. 5Wale wanao mtazama yeye wana furaha, na nyuso zao hazina aibu. 6Huyu mtu aliye onewa alilia na Yahwe akamsikia na kumuokoa kwenye matatizo yake yote. 7Malaika wa Yahwe huweka kambi wakiwazunguka wale wanao muogopa yeye na kuwaokoa. 8Onjeni muone Yahwe ni mzuri. Amebarikiwa mtu yule ambaye Yahwe ni kimbilio lake.

Injili

Yn 3:16–21

16Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, kwamba akamtoa mwanae wa pekee, ili kwamba mtu yeyote amwaminiye asiangamie bali awe na uzima wa milele. 17Kwa sababu Mungu hakumtuma mwanae duniani ili auhukumu ulimwengu, bali kwamba ulimwengu uokolewe katika yeye. 18Amwaminiye Yeye hatahukumiwa. Yeye asiyemwamini tayari ameshahukumiwa kwa sababu hajaliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. 19Hii ndiyo sababu ya hukumu, ya kwamba nuru imekuja ulimwenguni, lakini wanadamu wakapenda giza zaidi ya nuru kwa sababu matendo yao yalikuwa maovu. 20kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru wala haji nuruni ili matendo yake yasije yakawekwa wazi. 21Lakini, yeye atendaye kweli huja kwenye nuru ili matendo yake yaonekane kwamba yametendwa kwa utiifu wa Mungu.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 7 Aprili

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki