Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 6 Aprili
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 6 Aprili 2027
Jumanne · Juma la 2 la Pasaka
Sikukuu na watakatifu
Jumanne ya Juma la 2 la Pasaka
Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: nyeupe
Masomo ya siku
Somo la kwanza
32Idadi kubwa ya wale walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja: na hakuna hata mmoja wao aliyesema kwamba chochote alichomiliki kilikuwa cha kwake mwenyewe; badala yake walikuwa na vitu vyote shirika. 33Kwa nguvu kubwa mitume walikuwa wakiutangaza ushuhuda wao kuhusu ufufuo wa Bwana Yesu, na neema kubwa ilikuwa juu yao wote. 34Hapakuwa na mtu yeyote miongoni mwao aliyepungukiwa na mahitaji, kwa sababu watu wote waliokuwa na hati za viwanja au nyumba, waliviuza na kuleta pesa ya vitu waliyokuwa wameuza 35na kuviweka chini ya miguu ya mitume. Na mgawanyo ulifanywa kwa kila muumini, kulingana na kila mmoja alivyokuwa na hitaji. 36Yusufu, mlawi, mtu kutoka Kipro, alipewa jina la Barnabasi na mitume (hiyo ikitafasiriwa, ni mwana wa faraja). 37Akiwa na shamba, aliliuza na akaleta fedha, akaziweka chini ya miguu ya mitume.
Wimbo wa katikati
1Yahwe anatawala; amevikwa adhama; Yahwe amejivika na kujifunga nguvu. Ulimwengu umeimalishwa; hauwezi kusogezwa. 2Kiti chako cha enzi kimeimarishwa nyakati za kale; umekuwepo siku zote. 5Amri zako makini ni za kuaminika sana; utakatifu huipamba nyumba yako, Yahwe, milele.
Injili
7Usishangae kwa sababu nilikuwambia, 'ni lazima kuzaliwa mara ya pili.' 8Upepo huvuma popote upendapo na sauti yake mwaisikia, lakini hamjui utokako wala uendako. Ndivyo ilivyo hali ya kila aliyezaliwa na roho. 9Nikodemo akajibu, kwa kusema, “Mambo haya yawezekanaje?” 10Yesu akamjibu, “Wewe u mwalimu wa Israeli, hata hauyajui mambo haya? 11Amini, amini, nakuambia, kile tunachokifahamu twakishuhudia kwa kile tulichokiona. Lakini hampokei ushuhuda wetu. 12Kama nimewambia mambo ya hapa duniani na hamuamini, mtawezaje kuamini kama nikiwambia mambo ya mbinguni? 13Maana hakuna aliyepanda juu kutoka mbinguni isipokuwa yeye aliyeshuka, Mwana wa Adamu. 14Kama vile Musa alivyomwinua nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu lazima ainuliwe, 15ili kwamba wote watakaomwamini wapate uzima wa milele.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki