Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Machi 2027 › 7 Machi

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 7 Machi 2027

Jumapili · Juma la 4 la Kwaresima

Sikukuu na watakatifu

Dominika ya 4 ya Kwaresima

Dominika · Rangi ya liturujia: waridi

Masomo ya siku

Somo la kwanza

2 Nya 36:14–16, 19–23

14Vilevile, viongozi wote wa makauhanai na wa watu hawakuwa waaminifu, na waliufuata uovu wa mataiafa. Waliigoshi nyumba ya Yahwe ambayo alikuwa ameitakasa katika Yerusalemu. 15Yahwe, Mungu wa babu zao, akatuma maneno kwao tena na tena kupitia wajumbe wake, kwa sababu alikuwa na huruma juu ya watu wake na juu ya sehemu anayoishi. 16Lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, wakayadharau maneno yake, na kuwackeka manabii wake, hadi hasira ya Yahwe ilipoinuka zidi ya watu wake, hadi pailipokosekana msaada. 19Wakaichoma moto nyumba ya Mungu, wakauangusha chini ukuta wa Yerusalemu, wakachoma ikulu zake zote, na wakaharibu vitu vizuri vyote ndani yake. 20Mfalme akawapeleka mbali Babeli wale waliokuwa wameoka na upanga. Wakawa watumishi kwa ajili yake na wanawe hadi utawala wa Waajemi. 21Hili lilitokea ili kulitimiza neno la Yahwe kwa kinywa cha Yeremia, hadi nchi itakapokuwa imefurahia mapumziko ya Sabato yake. Iliishika Sabato kwa muda mrefu hadi kukataliwa kwake, ili miaka sabini itimie katika namna hii. 22Sasa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la Yahwe kwa kinywa cha Yeremia liweze kutimizwa, Yahwe akaipa hamasa roho ya Koreshi, mfalme wa Uajemi, kwamba akafanya tangazo katika uflme wake wote, na akaliweka pia katika maandishi. Akasema, 23“Hivi ndivyo Koreshi, mfalme wa Uajemi, anasema: Yahwe, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia. Ameniagiza nijenge nyumbaa kwa ajili yake katika Yerusalemu, ambao upo Yuda. Yeyote aliyemiongoni mwenu kutoma katika watu wake wote, Yahwe Mungu wenu, awe naye. Aende kwenye ile nchi.”

Wimbo wa katikati

Zab 137:1–6

1Kando ya mito ya Babeli tuliketi na tulilia tulipokumbuka kuhusu Sayuni. 2Tulitundika vinubi vyetu kwenye miti ya Babylon. 3Huko watekaji wetu walitaka tuwaimbie, na wale walio tudhihaki walitutaka sisi tufurahi, wakisema, “Tuimbieni moja ya nyimbo za Sayuni.” 4Tungewezaje kuimba wimbo unaomuhusu Yahwe katika nchi ya ugeni? 5Kama nikikusahau wewe, Yerusalemu, basi mkono wangu wa kuume na usahau ujuzi wake. 6Ulimi wangu na ushikamane juu ya kinywa changu kama nisipokufikiria tena, na kama sipendelei zaidi Yerusalemu kuliko furaha yangu kuu.

Somo la pili

Efe 2:4–10

4Lakini Mungu ni mwingi wa rehema kwa sababu ya pendo lake kubwa alilotupenda sisi. 5Wakati tulipokuwa wafu katika makosa yetu, alituleta pamoja katika maisha mapya ndani ya Kristo. Ni kwa neema kwamba mmeokolewa. 6Mungu alitufufua pamoja na kutufanya kukaa pamoja katika mahali pa mbingu ndani ya Kristo Yesu. 7Alifanya hivi ili katika nyakati zijazo aweze kutuonesha utajiri mkuu wa neema yake. Hutuonesha sisi hili kwa njia ya wema wake ndani ya Kristo Yesu. 8Kwa neema mmeokolewa kwa njia ya imani. Na hii haikutoka kwetu. Ni zawadi ya Mungu. 9Haitokani na matendo. Matokeo yake, asiwepo mmoja wapo wa kujisifu. 10Kwa sababu sisi tu kazi ya Mungu, tumeumbwa katika Kristo Yesu kutenda matendo mema. Ni matendo haya ambayo Mungu aliyapanga tangu zamani za kale kwa ajili yetu, ili tutembee katika hayo.

Injili

Yn 3:14–21

14Kama vile Musa alivyomwinua nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu lazima ainuliwe, 15ili kwamba wote watakaomwamini wapate uzima wa milele. 16Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, kwamba akamtoa mwanae wa pekee, ili kwamba mtu yeyote amwaminiye asiangamie bali awe na uzima wa milele. 17Kwa sababu Mungu hakumtuma mwanae duniani ili auhukumu ulimwengu, bali kwamba ulimwengu uokolewe katika yeye. 18Amwaminiye Yeye hatahukumiwa. Yeye asiyemwamini tayari ameshahukumiwa kwa sababu hajaliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. 19Hii ndiyo sababu ya hukumu, ya kwamba nuru imekuja ulimwenguni, lakini wanadamu wakapenda giza zaidi ya nuru kwa sababu matendo yao yalikuwa maovu. 20kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru wala haji nuruni ili matendo yake yasije yakawekwa wazi. 21Lakini, yeye atendaye kweli huja kwenye nuru ili matendo yake yaonekane kwamba yametendwa kwa utiifu wa Mungu.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 7 Machi

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki