Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Februari 2027 › 20 Februari
Kalenda ya Kiorthodoksi · 7 Februari (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 20 Februari 2027
Jumamosi · Wiki ya 38 baada ya Pentekoste · Sauti ya 4
Sikukuu na watakatifu
Baada ya Sikukuu ya Kuingia kwa Bwana Hekaluni
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
11Usemi huu ni wakuaminika: “Ikiwa tumekufa pamoja naye, tutaishi pamoja naye pia, 12kama tukivumilia, tutatawala pamoja naye pia, kama tukimkana yeye, naye pia atatukana sisi. 13kama hatutakuwa waaminifu, yeye atabaki kuwa mwaminifu, maana hawezi kujikana mwenyewe.” 14Endelea kuwakumbusha juu ya mambo haya. Waonye mbele za Mungu waache kubishana kuhusu maneno. Kwa sababu hakuna manufaa katika jambo hili. Kutokana na hili kuna uharibifu kwa wale wanaosikiliza. 15Fanya bidii kujionesha kuwa umekubalika kwa Mungu kama mtenda kazi asiye na sababu ya kulaumiwa. Litumie neno la kweli kwa usahihi. 16Jiepushe na majadiliano ya kidunia, ambayo huongoza kwa zaidi na zaidi ya uasi. 17Majadiliano yao yatasambaa kama donda ndugu. Miongoni mwao ni Himenayo na Fileto. 18Hawa ni watu walioukosa ukweli. Wanasema ya kuwa ufufuo tayari umishatokea. Wanapindua imani ya baadhi ya watu. 19Hata hivyo, msingi imara wa Mungu unasimama, wenye uandishi huu, “Bwana anawajua walio wake, na kila alitajaye jina la Bwana ni lazima ajitenge na udhalimu.”
Injili
2akaisema, 'Kulikuwa na hakimu katika mji fulani, ambaye hakuwa anamwogopa Mungu na hakuwaheshimu watu. 3Kulikuwa na mjane katika jiji hilo, naye alimwendea mara nyingi, akisema, 'Nisaidie kupata haki dhidi ya mpinzani wangu.' 4Kwa muda mrefu hakuwa tayari kumsaidia, lakini baada ya muda akasema moyoni mwake, 'Ingawa mimi simwogopi Mungu au kuheshimu mtu, 5lakini kwa vile huyu mjane ananisumbua nitamsaidia kupata haki yake, ili asije akanichosha kwa kunijia mara kwa mara. '' 6Kisha Bwana akasema, 'Sikiliza alivyosema huyo hakimu dhalimu. 7Je Mungu pia hataleta haki kwa wateule wake ambao wanamlilia mchana na usiku? Je, yeye hatakuwa mvumilivu kwao? 8Nawaambia kwamba ataleta haki kwao upesi. Lakini wakati Mwana wa Adamu atakapokuja, je, atakuta imani duniani? '
Watakatifu wa siku
- Mtakatifu Mtawa Parthenio, Askofu wa Lampsako (karne ya 4)
- Mtakatifu Mtawa Luka wa Ugiriki (karibu 946)
- Mfiadini wa Kikasisi Aleksanda, padri (1938)
- Mfiadini wa Kikasisi Aleksi, padri (1942)
- Wafiadini 1003 wa Nikomedia (303)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 7 Februari katika kalenda ya kanisa ni 20 Februari katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki