Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Februari 2027 › 19 Februari
Kalenda ya Kiorthodoksi · 6 Februari (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 19 Februari 2027
Ijumaa · Wiki ya 38 baada ya Pentekoste · Sauti ya 4
Sikukuu na watakatifu
Baada ya Sikukuu ya Kuingia kwa Bwana Hekaluni
Siku ya mfungo
Samaki wanaruhusiwa
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
1Simon Petro, Mtumwa na Mtume wa Yesu Kristo, Kwa wale walioipokea imani ile ile ya thamani kama tulivyoipokea sisi, imani iliyo ndani ya haki ya Mungu na mwokozi wetu Yesu Kristo. 2Neema iwe kwenu; amani iongezeke kupitia maarifa ya Mungu na Bwana wetu Yesu. 3Kupitia maarifa ya Mungu tumepata mambo yake yote kwa ajili ya uchaji wamaisha, Toka kwa Mungu aliyetuita kwa ajili ya uzuri wa utukufu wake. 4Kwa njia hii alitutumainishia ahadi kuu za thamani. Alifanya hili ili kutufanya warith wa asili ya Mungu, kwa kadiri tunavyoendelea kuuacha uovu wa dunia hii. 5Kwa sababu hii, fanyeni bidii kuongeza uzuri kwa njia ya imani yenu, kwa sababu ya uzuri, maarifa. 6Kupitia maarifa, kiasi, na kupitia kiasi saburi, na kupitia saburi, utauwa. 7Kupitia utauwa upendo wa ndugu na kupitia upendo wa ndugu, upendo. 8Kama mambo haya yamo ndani yenu, yakiendelea kukua ndani yenu, basi ninyi hamtakuwa tasa au watu msiozaa matunda katika maarifa ya Bwana wetu Yesu Kristo. 9Lakini yeyote asiyekuwa na mambo haya, huyaona mambo ya karibu tu; yeye ni kipofu. amesahau utakaso wa dhambi zake za kale. 10Kwa hiyo, ndugu zangu, fanyeni juhudi ili kujihakikishia uteule na wito kwa ajili yenu. Kama mtayafanya haya, hamtajikwaa.
Injili
1Yesu alipokuwa akitembea kutoka hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake akamwuliza, “Mwalimu, tazama mawe haya yakushangaza na majengo!” 2Akamwambia, Unaona majengo haya makubwa? Hakuna hata jiwe moja litakalo salia juu ya jingine ambalo halitaangushwa chini”. 3Naye alipokuwa amekaa juu ya Mlima wa Mizeituni nyuma ya hekalu, Petro, Yakobo, Yohana na Andrea wakamwuliza kwa siri, 4“Tuambie, mambo haya yatakuwa lini? Ni nini dalili ya mambo haya kutokea?” 5Yesu alianza kuwaambia, “Kuweni makini kwamba mtu yoyote asiwapotoshe. 6Wengi watakuja kwa jina langu wakisema, 'Mimi ndiye', na watawapotosha wengi. 7Mtakaposikia vita na tetesi za vita, msiogope; mambo haya hayana budi kutokea, lakini mwisho bado. 8Taifa litainuka kinyume na taifa jingine, na ufalme kinyume na ufalme. Patakuwa na matetemeko sehemu mbalimbali, na njaa. Huu ni mwanzo wa utungu.
Watakatifu wa siku
- Mtakatifu Mtawa Bukolo, Askofu wa Smirna (karibu 100)
- Mfiadini wa Kikasisi Demetrio, padri, na Mfiadini Anatoli (1921)
- Mfiadini wa Kikasisi Basili, padri (1930)
- Mfiadini wa Kikasisi Aleksanda, padri (1938)
- Wafiadini Dorothea bikira, wanawake Kristina na Kalista, na Mfiadini Theofilo (288-300)
- Mfiadini Fausta bikira na Wafiadini Evilasio na Maksimo (305-311)
- Mfiadini Yuliani wa Emesa (312)
- Watakatifu Watawa Barsanufio Mkuu na Yohana Nabii (karne ya 6)
- Askofu Mtakatifu Fotio, Patriarki wa Konstantinopoli (891)
- Wafiadini Martha na Maria, mabikira, na ndugu yao, Mtawa Mfiadini Likarioni, kijana
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 6 Februari katika kalenda ya kanisa ni 19 Februari katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki