Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Februari 2027 › 20 Februari

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 20 Februari 2027

Jumamosi · Juma la 1 la Kwaresima

Sikukuu na watakatifu

Jumamosi ya Juma la 1 la Kwaresima

Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: zambarau

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Kum 26:16–19

16Leo Yahwe Mungu wako anawaamuru kuzitii sheria na amri hizi; basi utazishikilia na kuzitenda kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote. 17Umetamka leo ya kuwa Yahwe ni Mungu wako, na kwamba utatembea katika njia zake na kushikilia sheria zake, maagizo yake na amri zake, na kwamba utaisikiliza sauti yake. 18Leo Yahwe ametamka ya kwamba mu watu ambao ni mali yake, kama alivyoahidi kwenu, na kwamba mnapaswa kushikilia amri zake zote. 19Na atawaweka juu zaidi ya mataifa mengine aliyoyaumba nanyi mtapokea sifa, umaarufu na heshima. Mtakuwa watu waliowekwa kando kwa Yahwe Mungu wako, kama alivyosema.”

Wimbo wa katikati

Zab 119:1–2, 4–5, 7–8

1Wamebarikiwa wale ambao njia zao hazina lawama, waenendao katika sheria ya Yahwe. 2Wamebarikiwa wale wazishikao amri zake thabiti, wamtafutao kwa moyo wao wote. 4Wewe umetuamuru kuyashika maagizo yako ili tuyachunguze kwa umakini. 5Oh, ningependa njia zangu ziwe thabiti nizitii amri zako! 7Nitakushukuru wewe kwa unyofu wangu wa moyo nijifunzapo amri za haki yako. 8Nitazitii amri zako; usiniache peke yangu.

Injili

Mt 5:43–48

43Mmesikia imenenwa, 'Umpende jirani yako, na umchukie adui yako.' 44Lakini nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanao waudhi, 45Ili kwamba muwe watoto wa baba yenu aliye mbinguni. Kwa kuwa anafanya jua liwaangazie wabaya na wema, na anawanyeshea mvua waovu na wema. 46Kama mkiwapenda wanaowapenda ninyi, mwapata thawabu gani? Kwani watoza ushuru hawafanyi hivyo? 47Na kama mkiwasalimia ndugu zenu tu mwapata nini zaidi ya wengine? Je!, Watu wa mataifa hawafanyi vivyo hivyo? 48Kwa hiyo yawapasa kuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Watakatifu wa 20 Februari

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki