Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Februari 2027 › 13 Februari

Kalenda ya Kiorthodoksi · 31 Januari (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 13 Februari 2027

Jumamosi · Wiki ya 37 baada ya Pentekoste · Sauti ya 3

Sikukuu na watakatifu

Wafiadini Kiro na Yohana, matabibu wasiopokea malipo, na pamoja nao Wafiadini Athanasia na binti zake Theodotia, Theoktista na Eudoksia (311)

Mfungo

Hakuna mfungo

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Waraka

1 The 5:14–23

14Twawasihi, ndugu: muwaonye wasio kwenda kwa utaratibu, watieni moyo walio kata tamaa, Wasaidieni walio wanyonge, na muwe wavumilivu kwa wote. 15Angalieni asiwepo mtu yeyote anayelipa baya kwa baya kwa mtu yeyote. Badala yake, fanyeni yaliyo mema kwa kila mmoja wenu na kwa watu wote. 16Furahini siku zote. 17Ombeni bila kukoma. 18Mshukuruni Mungu kwa kila jambo, kwa sababu hayo ndiyo mapenzi ya Mungu kwenu katika Yesu Kristo. 19Msimzimishe Roho. 20Msiudharau unabii. 21Yajaribuni mambo yote. Mlishike lililo jema. 22Epukeni kila mwonekano wa uovu. 23Mungu wa amani awakamilishe katika utakatifu. Roho, nafsi na mwili vitunzwe pasipo mawaa katika kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.

Waraka (Watakatifu Kiro na Yohana)

1 Kor 12:27–13:8

27Sasa ninyi ni mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake. 28Na Mungu ameweka katika kanisa kwanza mitume, pili manabii, tatu waalimu, kisha wale wote watendao matendo makuu, kisha karama za uponyaji, wale wasaidiao, wale wafanyao kazi ya kuongoza, na wote walio na aina mbalimbali za lugha. 29Je sisi sote ni mitume? Sisi sote ni manabii? Sisi sote ni waalimu? Je sisi sote tunafanya matendo ya miujiza? 30Je sisi sote tuna karama ya uponyaji? Sisi sote tunaongea kwa lugha? Sisi sote tunatafsiri lugha? 31Tafuteni sana karama zilizo kuu. Nami nitawaonesha njia iliyo bora zaidi. 13:1Tuseme kwamba ninanena kwa lugha za wanadamu na za malaika. Lakini kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo au upatu uvumao. 2Na kwamba nina karama ya unabii na ufahamu wa kweli zilizofichika na maarifa, na kwamba ninayo imani ya kuhamisha milima. Lakini ikiwa sina upendo, mimi si kitu. 3Na tuseme kwamba ninatoa milki yangu yote na kuwalisha masikini, na kwamba ninautoa mwili wangu ili nichomwe moto. Lakini kama sina upendo, hainifaidii kitu. 4Upendo huvumilia na hufadhili. Upendo haujisifu au kujivuna. Hauna kiburi 5au ukorofi. Hautafuti mambo yake, hauoni uchungu haraka, wala hauhesabu mabaya. 6Haufurahii udhalimu. Badala yake, hufurahi katika kweli. 7Upendo huvumilia mambo yote; huamini mambo yote, una ujasiri katika mambo yote, na hustahimili mambo yote. 8Upendo haukomi. Ikiwa kuna unabii, wote utapita. Ikiwa kuna lugha, zitakoma. Ikiwa kuna maarifa, yatapita.

Injili

Lk 17:3–10

3Jilindeni. Kama ndugu yako akikukosea mwonye, naye akitubu msamehe. 4Kama akikukosea mara saba kwa siku moja na mara saba kwa siku moja akaja kwako akisema, 'ninatubu,' msamehe!” 5Mitume wake wakamwambia Bwana, “tuongezee imani yetu.” 6Bwana akasema, “kama mgekuwa na imani kama punje ya haradarii, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu, 'n'goka na ukaote baharini,' nao ungewatii. 7Lakini nani miongoni mwenu, ambaye ana mtumishi anayelima shamba au anayechunga kondoo, atamwambia arudipo shambani, 'Njoo haraka na keti ule chakula? 8Je hatamwambia, 'Niandalie chakula nile, na jifunge mkanda na unitumikie mpaka nitakapo maliza kula na kunywa. Baada ya hapo uta kula na kunywa? 9Hata mshukuru mtumishi huyo kwasababu katimiza yale aliyoamriwa? 10Vivyo hivyo nanyi mkiisha kufanya mliyoagizwa semeni 'Sisi tu watumishi tusiostahili. Tumefanya tu yale tuliyopaswa kufanya.'

Injili (Watakatifu Kiro na Yohana)

Mt 10:1, 5–8

1Yesu akawaita wanafunzi wake kumi na wawili pamoja na kuwapa mamlaka juu ya pepo wachafu, kuwakemea na kuwafukuza na kuponya aina zote za maladhi na aina zote za magonjwa. 5Hawa kumi na wawili Yesu aliwatuma. Naye aliwaelekeza akisema “Msiende sehemu wanakoishi wamataifa na msiingie kwenye miji ya wasamalia. 6Badala yake, mwende kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israel. 7Na mnapokwenda, hubirini na kusema, ufalme wa mbinguni umekaribia.' 8Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma na fukuzeni pepo. Mmepokea bure, toeni bure.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 13 Februari

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 31 Januari katika kalenda ya kanisa ni 13 Februari katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki