Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2026 › 23 Desemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 10 Desemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 23 Desemba 2026
Jumatano · Wiki ya 30 baada ya Pentekoste · Sauti ya 4
Sikukuu na watakatifu
Wafiadini Mina, Hermogeni na Evgrafo (karibu 313)
Mfungo wa Kuzaliwa kwa Bwana
Mfungo: chakula kilichopikwa bila mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
1Kwa vile sheria ni kivuli cha mambo mema yajayo, si yale yaliyo halisi. Sheria kamwe haiwezi kuwakamilisha wale ambao wanaomkaribia Mungu kwa njia ya dhabihu zilezile ambazo makuhani waliendelea kutoa mwaka baada ya mwaka. 2Au vinginevyo dhabihu hizo zisingeweza kukoma kutolewa? Kwa kigezo hicho waabuduo, wakiwa wamesafishwa mara moja, wasingelikuwa na utambuzi zaidi wa dhambi. 3Bali katika dhabihu hizo kuna ukumbusho wa dhambi zilizotendwa mwaka baada ya mwaka. 4Kwa kuwa haiwezekani kwa damu ya mafahari na mbuzi kuziondoa dhambi. 5Wakati Kristo alipokuja duniani, alisema, “Hamkutamani matoleo au dhabihu, badala yake, mliandaa mwili kwa ajili yangu. 6Hamkuwa na thamani katika matoleo yote ya kuteketezwa au dhabihu kwa ajili ya dhambi. 7Kisha nilisema, “Ona, hapa ninayafanya mapenzi yako, Mungu, kama ilivyoandikwa kunihusu mimi katika gombo”. 8Alisema kama ilivyo semwa hapo juu: “Hamkutamani dhabihu, matoleo, au sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya dhambi, wala hukuona furaha ndani yake” dhabihu ambazo zinatolewa kulingana na sheria. 9Kisha alisema, “Ona, niko hapa kufanya mapenzi yako”. Ameweka pembeni taratibu zilizo za awali ili kuimarisha zile za pili. 10Katika taratibu za pili, tumekwisha tengwa kwa Mungu kwa mapenzi yake kupitia kujitoa kwa mwili wa Yesu Kristo mara moja kwa nyakati zote. 11Ni kweli, kila kuhani husimama kwa huduma siku kwa siku, akitoa dhabihu ile ile, ambayo, kwa vyovyote, kamwe isingeweza kuziondoa dhambi. 12Lakini baada ya Kristo kutoa dhabihu mara moja kwa dhambi milele yote, aliketi mkono wa kuume wa Mungu, 13akisubiri mpaka maadui zake watiwe chini na kufanywa kiti kwa ajili ya miguu yake. 14Kwa kuwa kwa njia ya toleo moja amewakamilisha milele wale ambao wametengwa kwa Mungu. 15Na Roho Mtakatifu pia ashuhudia kwetu. Kwa kuwa kwanza alisema, 16“Hili ni agano nitakalofanya pamoja nao baada ya siku hizo; asema Bwana: nitaweka sheria zangu ndani ya mioyo yao, na nitaziandika katika akili zao”. 17Kisha alisema, “Hawatazikumbuka tena dhambi na matendo yao mafu”. 18Sasa mahali palipo na msamaha kwa hawa, hakuna tena dhabihu yoyote kwa ajili ya dhambi.
Injili
5Wakati wengine walipokuwa wakisema juu ya hekalu, namna lilivyokuwa limepambwa na mawe mazuri na matoleo, alisema, 6“Kwa habari ya mambo haya mnayoyaona, siku zitakuja ambazo hakuna jiwe moja ambalo litaachwa juu ya jiwe jingine ambalo halitabomolewa.” 7Hivyo wakamuuliza, wakasema, “Mwalimu, mambo haya yatatokea lini? Na nini ni itakuwa ishara kwamba haya mambo yako karibu kutokea?” 10Kisha akawaambia, “Taifa litainuka kupigana na taifa jingine, na ufalme juu ya ufalme mwingine. 11Kutakuwa na matetemeko makubwa, na njaa na tauni katika maeneo mbalimbali. Kutakuwa na matukio ya kutisha na ishara za kutisha kutoka mbinguni. 20Mtakapoona Yerusalemu imezungukwa na majeshi, basi jueni kwamba uharibifu wake umekaribia. 21Hapo wale walioko Yudea wakimbilie milimani, na wale walioko katikati ya jiji waondoke, na msiwaache walioko vijijini kuingia. 22Maana hizi ni siku za kisasi, ili kwamba mambo yote yaliyoandikwa yapate kutimilika. 23Ole ni kwa wale walio na mimba na kwa wale wanyonyeshao katika siku hizo! Kwa maana kutakuwa na adha kuu juu ya nchi, na ghadhabu kwa watu hawa. 24Na wataanguka kwa ncha ya upanga na watachukuliwa mateka kwa mataifa yote, na Yerusalem itakanyagwa na watu wa mataifa, mpaka wakati wa watu wa mataifa utakapotimilika.
Watakatifu wa siku
- Askofu Mtakatifu Yoasafu, Askofu wa Belgorod (1754)
- Wafiadini wa Kikasisi Yakobo na Aleksanda, mapadri, Mfiadini wa Kikasisi Evgraf, padri, na mwanawe (1918)
- Wafiadini wa Kikasisi Anatoli, Aleksanda, Eugenio, Konstantino, Nikolao, mapadri, na pamoja nao Wafiadini Petro, Eusebio, Mikaeli, Dorotheo, Laurenti, Gregori, na Wafiadini Aleksandra na Tatiana (1937)
- Mfiadini wa Kikasisi Mikaeli, padri (1937)
- Mtawa Mfiadini Sergio (1937)
- Mfiadini Eudokia (baada ya 1937)
- Wafiadini wa Kikasisi Nikolao na Aleksi, mapadri (1938)
- Watakatifu Ana na Tatiana Waungamaji (1948)
- Mtakatifu Thekla Mwungamaji (1954)
- Mtakatifu Mtawa Ana Mwungamaji (1958)
- Mfiadini Gemelo wa Paflagonia (karibu 361)
- Mtakatifu Mtawa Tomaso (karibu 886-912)
- Wabarikiwa Yohana (1503) na wazazi wake Stefano (1446) na Angelina, wa familia ya Branković, watawala wa Serbia
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 10 Desemba katika kalenda ya kanisa ni 23 Desemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki