Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2026 › 24 Desemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 11 Desemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 24 Desemba 2026
Alhamisi · Wiki ya 30 baada ya Pentekoste · Sauti ya 4
Sikukuu na watakatifu
Mtakatifu Mtawa Danieli, mkaa nguzoni (489-490)
Mfungo wa Kuzaliwa kwa Bwana
Mfungo: pamoja na mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
35Kwa hiyo msiutupe ujasiri wenu, ulio na zawadi kuu. 36Kwa kuwa mnahitaji uvumilivu, ili kwamba mpate kupokea ambacho Mungu amekiahidi, baada ya kuwa mmekwisha yatenda mapenzi yake. 37Kwa kuwa baada ya kitambo kidogo, mmoja anayekuja, atakuja hakika na hatakawia. 38Mwenye haki wangu ataishi kwa imani. Kama atarudi nyuma, sitapendezwa naye.” 39Lakini sisi si kama wale warudio nyuma kwa kuangamia. Badala yake, sisi ni baadhi ya wale tulio na imani ya kuzilinda roho zetu. 11:1Sasa imani ni hakika aliyo nayo mtu wakati atarajiapo kitu fulani kwa ujasiri. Ni hakika ya kitu ambacho bado hakijaonekana. 2Kwa sababu hii mababu zetu walithibitika kwa imani yao. 3Kwa imani tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa amri ya Mungu, ili kwamba kile kinachoonekana hakikutengenezwa kutokana na vitu ambavyo vilikuwa vinaonekana. 4Ilikuwa kwa sababu ya imani kwamba Habili alimtolea Mungu sadaka ya kufaa kuliko alivyofanya Kaini. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba alisifiwa kuwa mwenye haki. Mungu alimsifu kwa sababu ya zawadi alizoleta. Kwa sababu hiyo, Habili bado ananena, ingawa amekufa. 5Ilikuwa kwa imani kwamba Enoko alichukuliwa juu na hakuona mauti. “Hakuonekana, kwa sababu Mungu alimchukua” kwa vile ilinenwa juu yake kuwa alimpendeza Mungu kabla ya kuchukuliwa juu. 6Pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa kuwa ajaye kwa Mungu lazima aamini kwamba Mungu anaishi na kwamba huwapatia zawadi wale wamtafutao. 7Ilikuwa ni kwa imani kwamba Nuhu, akiwa ameonywa na Mungu kuhusiana na mambo ambayo hayakuwa yameonekana, kwa heshima ya ki Mungu alitengeneza safina kwa ajili ya kuiokoa familia yake. Kwa kufanya hivi, aliuhukumu ulimwengu na akawa mrithi wa haki ambayo huja kupitia imani.
Injili
28Lakini mambo haya yatakapoanza kutokea, simameni, inueni vichwa vyenu, kwa sababu ukombozi wenu umesogea karibu.” 29Yesu akawaambia kwa mfano, “Uangalieni mtini, na miti yote. 30Inapotoa machipukizi, mnajionea wenyewe na kutambua kwamba kiangazi tayari kiko karibu. 31Vivyo hivyo, mnapoona mambo haya yanatokea, ninyi tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu umekaribia. 32Kweli, nawaambieni, kizazi hiki hakitapita, mpaka mambo haya yote yatakapotokea. 33Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Watakatifu wa siku
- Mfiadini wa Kikasisi Theofani, Askofu wa Solikamsk, na pamoja naye wafiadini wa kikasisi wawili na wafiadini watano (1918)
- Mfiadini wa Kikasisi Nikolao, padri (1937)
- Mfiadini wa Kikasisi Yohana, padri (1941)
- Mfiadini Mirakso (karne ya 7)
- Mtakatifu Mtawa Luka, mkaa nguzoni (970-980)
- Mtakatifu Mtawa Nikoni, aliyekonda, wa Mapango ya Kyiv (karne ya 12)
- Wafiadini Akepsio na Aithala
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 11 Desemba katika kalenda ya kanisa ni 24 Desemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki