Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2026 › 22 Desemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 22 Desemba 2026
Jumanne · Juma la 4 la Majilio
Sikukuu na watakatifu
22 Desemba
Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: zambarau
Masomo ya siku
Somo la kwanza
24Alipokuwa amemwachisha kunyonya, alimbeba, akimchukua pamoja ng'ombe dume wa miaka mitatu, unga kama kilo thelathini na chupa ya mvinyo, akampeleka katika nyumba ya BWANA huko Shilo. Na mtoto huyo alikuwa bado mdogo. 25Walimchinja yule ng'ombe, na wakamkabidhi mtoto kwa Eli. 26Akasema, “Ee bwana wangu! Kama uishivyo, bwana wangu, Mimi ndiye yule mwanamke niliyesimama hapa karibu nawe nikimwomba BWANA. 27Niliomba kwa ajili ya mtoto huyu na BWANA akawa amenijibu ombi la dua yangu nililomwomba. 28Nami nimemtoa kwa BWANA; kwa maisha yake yote, nimempa BWANA.” Ndipo Elikana na familia yake wakamtukuza BWANA huko Shilo.
Wimbo wa katikati
1Hana aliomba akasema, “moyo wangu wamtukuza BWANA. Pembe yangu imejulikana katika BWANA. Kinywa changu kinatamba dhidi ya maadui zangu, kwa kuwa naufurahia wokovu wako. 4Pinde za mashujaa zimevunjika, bali wale wanaojikwaa hujivika nguvu kama mshipi. 5Wale walio na shibe ya kutosha wamejikodisha ili wapate chakula; wale waliokuwa na njaa hawana njaa tena. Hata yule aliye kuwa tasa amezaa watoto saba, bali mwanamke mwenye watoto wengi amenyong'onyea. 6BWANA huua na huuisha. Hushusha kuzimu na huleta tena juu. 7BWANA humfanya maskini, na yeye ndiye humtajirisha mtu. Yeye hudhili, lakini pia hukweza 8Yeye humwinua juu maskini toka mavumbini: Huwainua wahitaji toka jalalani na kuwaketisha pamoja na wakuu na kuwarithisha kiti cha enzi cha utukufu. Kwa kuwa nguzo za dunia ni za BWANA na ameukalisha ulimwengu juu yake.
Injili
46Mariamu akasema, nafsi yangu inamsifu Bwana, 47na roho yangu imefurahi katika Mungu Mwokozi wangu. 48Kwa maana ameiangalia hali ya chini ya mtumishi wake wa kike. Tazama, tangu sasa katika vizazi vyote wataniita mbarikiwa. 49Kwa maana yeye aliyemweza amefanya mambo makubwa kwangu, na jina lake ni takatifu. 50Rehema yake inadumu toka kizazi hata kizazi kwa wale wanao mheshimu yeye. 51Ameonesha nguvu kwa mkono wake; amewatawanya wale ambao walijivuna juu ya mawazo ya mioyo yao. 52Amewashusha chini wana wa wafalme toka katika viti vyao vya enzi na kuwainua juu walio na hali ya chini. 53Aliwashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri, bali matajiri amewafukuza mikono mitupu. 54Ametoa msaada kwa Israeli mtumishi wake, ili kukumbuka kuonesha rehema 55(kama alivyosema kwa baba zetu) kwa Abrahamu na uzao wake milele.” 56Mariamu alikaa na Elizabeti yapata miezi mitatu hivi ndipo akarudi nyumbani kwake.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki