Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2026 › 21 Desemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 8 Desemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 21 Desemba 2026
Jumatatu · Wiki ya 30 baada ya Pentekoste · Sauti ya 4
Sikukuu na watakatifu
Mtakatifu Mtawa Patapio (karne ya 7)
Mfungo wa Kuzaliwa kwa Bwana
Mfungo: chakula kilichopikwa bila mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
7Hivyo kama agano la kwanza lisingekuwa na makosa, ndipo hakungekuwa na haja kutafuta agano la pili. 8Kwa kuwa wakati Mungu alipogundua makosa kwa watu alisema, “Tazama, siku zinakuja, 'asema Bwana, 'wakati nitakapotengeneza agano jipya pamoja na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. 9Halitakuwa kama agano nililofanya pamoja na baba zao siku ambayo niliwachukua kwa mkono kuwaongoza kutoka nchi ya Misri. Kwa kuwa hawakuendelea katika agano langu, nami sikuwajali tena,' asema Bwana. 10Kwa kuwa hili ndilo agano nitafanya kwa nyumba ya Israeli baada ya siku hizo,' asema Bwana. 'nitaweka sheria zangu mawazoni mwao, na nitaziandika mioyoni mwao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 11Hawatafundishana kila mmoja na jirani yake, na kila mmoja na ndugu, yake, akisema, “Mjue Bwana,” hivyo wote watanijua mimi, kutoka mdogo hadi mkubwa wao. 12Hivyo nitaonyesha rehema kwa matendo yao yasiyo ya haki, na sizitazikumbuka dhambi zao tena.” 13Kwa kusema “Mpya,” amelifanya agano la kwanza kuwa kuukuu. Na hilo ambalo amelitangaza kuwa kuukuu liko tayari kutoweka.
Injili
27Baadhi ya Masadukayo wakamwendea, wale ambao wanasema kwamba hakuna ufufuo, 28wakamwuliza, wakisema, “Mwalimu, Musa alituandikia kwamba kama mtu akifiwa na ndugu mwenye mke ambaye hana mtoto basi anapaswa kumchukuna mke wa ndugu yake na kuzaa nae kwa ajili ya kaka yake. 29Kulikuwa na ndugu saba Wa kwanza alioa, akafa bila kuacha mtoto, 30na wa pili pia. 31Wa tatu akamchukua vilevile, vivyo hivyo wa saba hakuacha watoto na akafa. 32Baadaye yule mwanamke pia akafa. 33Katika ufufuo atakuwa mke wa nani? Maana wote saba walikuwa wamemwoa. ' 34Yesu akawaambia, “Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa. 35Lakini wale wanastaohili kupokea ufufuo wa wafu na kuingia uzima wa milele hawaoi wala hawaolewi. 36Wala hawawezi kufa tena, kwa sababu huwa sawasawa na malaika na ni watoto wa Mungu, wana wa ufufuo. 37Lakini hiyo wafu wanafufuliwa, hata Musa alionyesha mahali katika habari za kichaka, pale alimwita Bwana kama Mungu wa Ibrahimu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo. 38Sasa, yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai, kwa sababu wote huishi kwake. “ 39Baadhi ya walimu wa Sheria wakamjibu, 'Mwalimu, umejibu vema. ' 40Hawakuthubutu kumwuliza maswali mengine zaidi. 41Yesu akawaambia, “Ki vipi watu wanasema kwamba Kristo ni mwana wa Daudi? 42Maana Daudi mwenyewe anasema katika Zaburi: Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti mkono wa kulia, 43mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako. ' 44Daudi anamwita Kristo 'Bwana', basi atakuwaje mwana wa Daudi?”
Watakatifu wa siku
- Mfiadini wa Kikasisi Sergio, padri (1937)
- Mitume Sosthene, Apolo, Kefa, Tikiko, Epafrodito, Kaisari na Onesiforo, wa Mitume 70 (karne ya 1)
- Wafiadini 62, mapadri, na walei 300, walioteswa na Waariani huko Afrika (477)
- Mtakatifu Mtawa Kirilo wa Chelmogorsk (1368)
- Mfiadini Anthusa huko Roma (karne ya 5)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 8 Desemba katika kalenda ya kanisa ni 21 Desemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki