Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2026 › 20 Desemba

Kalenda ya Kiorthodoksi · 7 Desemba (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 20 Desemba 2026

Jumapili · Sauti ya 4

Sikukuu na watakatifu

Jumapili ya 29 baada ya Pentekoste

Mfungo wa Kuzaliwa kwa Bwana

Samaki wanaruhusiwa

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Injili ya 7 ya Sala ya Alfajiri

Yn 20:1–10

1Mapema siku ya kwanza ya juma, kungali bado giza, Mariamu Magdalena alikuja kaburini; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini. 2Kwa hiyo akakimbia mbio kwenda kwa Simon Petro na kwa yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, kisha akawaambia, “wamemchukua Bwana kaburini, nasi hatujui kule walikomlaza.” 3Kisha Petro na yule mwanafunzi mwingine wakatoka, kuelekea kaburini. 4Wote walipiga mbio kwa pamoja; yule mwanafunzi mwingine alikimbia kwa kasi zaidi ya Petro nakufika kaburini wa kwanza. 5Akasimama na kisha kuangalia kaburini; akaiona ile sanda ya kitani imelala, lakini hakuingia ndani. 6Kisha Simon Petro naye akafika akaingia ndani ya Kaburi. Akaiona ile sanda ya kitani imelala pale 7na ile leso iliyokuwa kichwani pake haikuwa imelala pamoja na zile sanda za kitani bali ilikuwa imelala pembeni peke yake. 8Ndipo yule mwanafunzi mwingine naye alipoingia ndani ya kaburi; akaona na kuamini. 9Kwa kuwa hadi wakati huo walikuwa bado hawajayajua maandiko kwamba ilimlazimu Yesu afufuke tena katika wafu. 10Kisha wanafunzi wakaenda tena nyumbani kwao.

Waraka

Kol 3:12–16

12Kama wateule wa Mungu, watakatifu na wapendwao, jivikeni utu wema, ukarimu, unyenyekevu, upole na uvumilivu. 13Chukulianeni ninyi kwa ninyi. Hurumianeni kila mtu na mwenzake. Kama mtu analalamiko dhidi ya mwingine, amsamehe kwa jinsi ilele ambayo Bwana alivyo wasamehe ninyi. 14Zaidi ya mambo haya yote, muwe na upendo, ambao ndio kigezo cha ukamilifu. 15Amani ya Kristo na iwaongoze mioyoni mwenu. Ilikuwa ni kwa ajili ya amani hii kwamba mliitiwa katika mwili mmoja. Iweni na shukrani. 16Na Neno la Kristo likae ndani yenu kwa utajiri. Kwa hekima yote, fundishaneni na kushauriana ninyi kwa ninyi kwa Zaburi, nyimbo, na nyimbo za rohoni. Imbeni kwa shukrani mioyo yenu kwa Mungu.

Injili

Lk 17:12–19

12Alipokua akiingia kwenye kijiji kimoja, huko alikutana na watu kumi waliokuwa na ukoma. Wakasimama mbali 13wakapaza sauti wakasema “Yesu, Bwana tuhurumie.” 14Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani.” nao walipokua wakienda wakatakasika. 15Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa sauti kuu akimsifu Mungu. 16Akapiga magoti miguuni mwa Yesu akamshukuru. Yeye alikua msamaria. 17Yesu akajibu, akasema, “Je hawakutakasika wote kumi? Wako wapi wale wengine tisa? 18Hakuna hata mmoja aliyeonekana kurudi ili kumtukuza Mungu, isipokuwa huyu mgeni?” 19Akamwambia, “Inuka na uende zako imani yako imekuponya.”

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 20 Desemba

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 7 Desemba katika kalenda ya kanisa ni 20 Desemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki