Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 28 Novemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 28 Novemba 2026
Jumamosi · Juma la 34 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumamosi ya Juma la 34 la Mwaka
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani
Kumbukumbu ya Bikira Maria siku ya Jumamosi · Kumbukumbu ya hiari
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1Kisha malaika akanionesha mto wa maji ya uzima, maji yalikuwa ya mng'ao kama wa bilauri. Yalikuwa yakitiririka kutoka katika kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana Kondoo 2Kupitia katikati ya mtaa wa mji. Katika kila pembe ya mto palikuwa na mti wa uzima, unaozaa aina kumi na mbili za matunda, na huzaa matunda kila mwezi. Majani ya mti ni kwa ajili ya uponyaji wa mataifa. 3Wala hapatakuwa na laana yoyote tena. Kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana Kondoo kitakuwemo ndani ya mji, na watumishi wake watamtumikia. 4Watamuona uso wake, na jina lake litakuwa juu ya vipaji vya nyuso zao. 5Hapatakuwa na usiku tena; wala hapatakuwa na hitaji la mwanga wa taa au jua kwa sababu Bwana Mungu ataangaza juu yao. Nao watatawala milele na milele. 6Malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kuaminika na kweli. Bwana Mungu wa roho za manabii alimtuma malaika wake kuwaonesha watumishi wake kitakachotokea hivi karibuni.” 7“Tazama! Ninakuja upesi! Amebarikiwa yeye anayeyatii maneno ya unabii wa kitabu hiki.”
Wimbo wa katikati
1Oh njoni, tumwimbie Yahwe; na tumwimbie kwa shangwe mwamba wa wokovu wetu. 2Tuingie uweponi mwake kwa shukrani; tumwimbie yeye kwa zaburi ya sifa. 3Kwa maana Yahwe ni Mungu mkuu na Mfalme mkuu juu ya miungu yote. 4Mkononi mwake zimo bonde za dunia; navyo vilele vya milima ni vyake. 5Bahari ni yake, maana aliiumba, na mikono yake ilitengeneza nchi kavu. 6Oh njoni, tumwabudu na tupige magoti; tupige magoti mbele za Yahwe, muumbaji wetu: 7Kwa maana yeye ni Mungu wetu, na sisi tu watu wa malisho yake na kondoo wa mkono wake. Ni heri leo mngesikia sauti yake!
Injili
34Lakini jiangalieni wenyewe, ili kwamba mioyo yenu isije ikalemewa na ufisadi, ulevi, na mahangaiko ya maisha haya. Kwa sababu ile siku itawajia ghafla 35kama mtego. Kwasababu itakuwa juu ya kila mmoja aishiye katika uso wa dunia nzima. 36Lakini mwe tayari wakati wote, mwombe kwamba mtakuwa imara vya kutosha kuyaepuka haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.”
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki