Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 19 Novemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 6 Novemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 19 Novemba 2026
Alhamisi · Wiki ya 25 baada ya Pentekoste · Sauti ya 7
Sikukuu na watakatifu
Askofu Mtakatifu Paulo Mwungamaji, Patriarki wa Konstantinopoli (350)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
13Lakini inatupasa tumshukuru Mungu kila mara kwa ajili yenu ndugu mpendwao na Bwana. Kwa sababu Bwana aliwachagua ninyi kama malimbuko ya wokovu kwa utakaso wa Roho na imani katika ile kweli. 14Hiki ndicho alichowaitieni ninyi, kwamba kupitia injili muweza kuupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo. 15Kwa hiyo, ndugu, simameni imara. Ueleweni ule utamaduni mliofundishwa, kwa neno au kwa barua yetu. 16Sasa, Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu Baba yetu aliyetupenda na kutupa faraja ya milele na ujasiri mwema kwa ajili ya maisha yajayo kupitia neema, 17awafariji na kuifanya imara mioyo yenu katika kila neno na kazi njema. 3:1Na sasa, ndugu, tuombeeni, kwamba neno la Bwana liweze kuenea na kutukuzwa, kama ilivyo pia kwenu. 2Ombeni kwamba tuweze kuokolewa kutoka katika uovu na watu waasi, kwa kuwa si wote wana imani. 3Lakini Bwana ni mwaminifu, ambaye atawaimarisha ninyi na kuwalinda kutoka kwa yule mwovu. 4Tunaujasiri katika Bwana kwa ajili yenu, kwamba mnatenda na mtaendelea kutenda mambo ambayo tunawaagiza. 5Bwana aweze kuongoza mioyo yenu katika upendo na katika uvumilivu wa Kristo.
Injili
47Ole wenu, kwa sababu mnajenga na kuweka kumbukumbu kwenye makaburi ya manabii' ambao waliuwawa na mababu zenu. 48Hivyo ninyi mwashuhudia na kukubaliana na kazi walizozifanya mababu zenu, kwa sababu hakika waliwauwa manabii ambao mnajenga kumbukumbu katika makaburi yao. 49Kwa sababu hiyo pia, hekima ya Mungu inasema, 'Nitawatumia manabii na mitume nao watawatesa na kuwaua baadhi yao. 50Kizazi hiki kitawajibika kwa damu ya manabii waliouawa tangu kuanza kwa dunia, 51Kutoka damu ya Abeli hadi damu ya Zakaria, aliyeuawa katikati ya madhabahu na patakatifu. Ndiyo, nawaambia ninyi, kizazi hiki kitawajibika. 52Ole wenu waalimu wa sheria za Kiyahudi, kwa sababu mmechukua funguo za ufahamu; nyie wenyewe hamuingii, na wale wanaotaka kuingia mnawazuia.” 53Baada ya Yesu kuondoka pale, Waandishi na Mafarisayo walimpinga na kubishana naye juu ya mambo mengi. 54wakijaribu kumnsana kwa maneno yake. 12:1Kwa wakati huo, maelfu mengi ya watu walikusanyika pamoja, kiasi cha kuanza kukanyagana, akaanza kusema na wanafunzi wake kwanza, “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo ambayo ni unafiki”
Watakatifu wa siku
- Mtakatifu Mtawa Barlaamu wa Khutyn (1192)
- Wafiadini wa Kikasisi Niketa, Askofu wa Orekhovo-Zuyevo, Anatoli, Arsenio, Nikolao, Nikolao, Konstantino, mapadri, Watawa Wafiadini Barlaamu, Gabrieli na Gabrieli, Watawa Wafiadini Nina na Serafima (1937)
- Mtakatifu Mtawa Luka wa Tauromenio (800-820)
- Mfiadini wa Kikasisi Basili, padri (1938)
- Wafiadini Tekusa, Aleksandra, Polaktia, Klaudia, Eufrosini, Athanasia na Matrona (karne ya 3)
- Kumbukumbu ya kupatikana kwa Msalaba wenye Thamani na misumari na Malkia Mtakatifu Helena Sawa na Mitume huko Yerusalemu (326)
- Mtakatifu Mtawa Luka, mtunza mali wa Mapango ya Kyiv (karne ya 13)
- Askofu Mtakatifu Germano, Askofu Mkuu wa Kazan (1567)
- Mtakatifu Mtawa Barlaamu wa Keret (karne ya 16)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 6 Novemba katika kalenda ya kanisa ni 19 Novemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki