Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 18 Novemba

Kalenda ya Kiorthodoksi · 5 Novemba (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 18 Novemba 2026

Jumatano · Wiki ya 25 baada ya Pentekoste · Sauti ya 7

Sikukuu na watakatifu

Wafiadini Galaktioni na Epistimia (karne ya 3)

Siku ya mfungo

Mfungo: pamoja na mafuta

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Waraka

2 The 2:1–12

1Sasa kuhusu kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kukusanywa pamoja ili tuwe naye: tunawaomba ninyi ndugu zetu, 2kwamba msisumbuliwe wala kutabishwa kwa urahisi, kwa roho, au kwa ujumbe au kwa barua inayoonkana kuwa imetoka kwetu, ikisema ya kuwa siku ya Bwana tayari imekuja. 3Mtu na asiwadanganye kwa namna yoyote. Kwa kuwa haitakuja mpaka lile anguko litokee kwanza na mtu wa uasi afunuliwe, yule mwana wa uharibifu. 4Huyu ndiye apingaye naye hujiinua mwenyewe akimpinga Mungu na chochote kinachoabudiwa. Na matokeo yake, hukaa kwenye hekalu la Mungu na kujionyesha yeye kuwa kama Mungu. 5Je, hamkumbuki kuwa nilipokuwa nanyi niliwaambia juu ya mambo haya? 6Sasa mnajua kile kinachomzuia, ili kwamba aweze kufunuliwa kwa wakati sahihi utakapowadia. 7Kwa kuwa siri ya yule mtu mwenye kuasi inafanya kazi mpaka sasa, ila tu kuna anaye mzuia sasa mpaka atakapotolewa njiani. 8Ndipo yule mwenye kuasi atakapofunuliwa, amabaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake. Bwana atamfanya kuwa si chochote kwa ufunuo wa ujio wake. 9Ujio wa yule mwenye kuasi utakuwa kwa sababu ya kazi ya shetani kwa nguvu zote, ishara na maajabu ya uongo, 10na uongo wote wenye udhalimu. Mambo haya yatakuwepo kwa wale wanaopotea, kwa sababu hawakuupokea upendo wa kweli kwa ajili ya kuokolewa kwao. 11Kwa sababu hiyo Mungu anawatumia kazi yenye uovu ili waamini uongo. 12Matokeo yake ni kwamba wote watahukumiwa, wale ambao hawakuamini ukweli bali wao hujifurahisha katika udhalimu.

Injili

Lk 11:42–46

42Lakini ole wenu Mafarisayo, kwani mnatoa zaka ya mnanaa na mchicha na kila aina ya mboga ya bustani. Lakini mmeacha mambo ya haki na kumpenda Mungu. Ni muhimu zaidi kufanya yaliyo ya haki na kumpenda Mungu, bila kuacha kufanya na hayo mengine pia. 43Ole wenu Mafarisayo, kwa kuwa mnapenda kukaa katika viti vya mbele kwenye masinagogi na kuamkiwa kwa salamu za heshima sokoni. 44Ole wenu, kwani mnafanana na makaburi yasiyo na alama ambayo watu hutembea juu yake pasipokujua.” 45Mwalimu mmoja wa sheria za Kiyahudi akamjibu na kumwambia, “Mwalimu, unachokisema kinatuudhi pia sisi.” 46Yesu akasema, “Ole wenu, waalimu wa sheria! kwani mnawapa watu mizigo mikubwa wasiyoweza kuibeba, walakini ninyi hamgusi mizigo hiyo hata kwa moja ya vidole vyenu.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 18 Novemba

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 5 Novemba katika kalenda ya kanisa ni 18 Novemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki