Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 16 Novemba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 16 Novemba 2026

Jumatatu · Juma la 33 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumatatu ya Juma la 33 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Mt. Gertrudi Mkuu, bikira · Kumbukumbu ya hiari

Mt. Margareta wa Scotland · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Ufu 1:1–4; 2:1–5

1Huu ni ufunuo wa Yesu Kristo ambao Mungu alimpa ili kuwaonesha watumishi wake mambo ambayo lazima yatokee karibuni. Aliyafanya yajulikane kwa kumtuma malaika wake kwa mtumishi wake Yohana. 2Yohana alitoa ushuhuda wa kila kitu alichoona kuhusiana na neno la Mungu na kwa ushuhuda uliotolewa kuhusu Yesu Kristo. 3Amebarikiwa yeye asomaye kwa sauti na wale wote wanaoyasikia maneno ya unabii huu na kutii kilichoandikwa humo, kwa sababu muda umekaribia. 4Yohana, kwa makanisa saba yaliyoko Asia: neema iwe kwenu na amani kutoka kwake aliyepo, aliyekuwepo, na atakayekuja, na kutoka kwa roho saba walio mbele ya kiti chake cha enzi, 2:1“Kwa malaika wa kanisa la Efeso andika: 'Haya ni maneno ya yule anayeshikilia zile nyota saba katika mkono wake wa kuume. Yeye atembeaye kati ya vinara vya dhahabu vya taa saba asema hivi, “ 2'“Najua ambacho umetenda na bidii yako ya kazi na uvumilivu wako thabiti, na kwamba huwezi kuhusiana nao walio waovu, na umewajaribu wote wanaojiita kuwa mitume na kumbe siyo, na wameonekana kuwa waongo. 3Najua una subira na uvumilivu, na umepitia mengi kwa sababu ya jina langu, na haujachoka bado. 4Lakini hili ndilo nililonalo dhidi yako, umeuacha upendo wako wa kwanza. 5Kwa hiyo kumbuka ulipoanguka, ukatubu na kufanya matendo uliyofanya tangu mwanzo. Usipotubu, nitakuja kwako na kukiondoa kinara chako kutoka mahali pake.

Wimbo wa katikati

Zab 1:1–4, 6

1Amebarikiwa mtu yule asiye enenda katika ushauri wa waovu, au kusimama katika njia ya wenye dhambi, au kukaa katika kusanyiko la wenye mizaha. 2Bali yeye huifurahia sheria ya Yahwe, na huitafakari sheria yake mchana na usiku. 3Atakuwa kama mti uliopandwa karibu na mkondo wa maji ambao huzaa matunda yake kwa majira yake, ambao majani yake hayakauki; lolote afanyalo litafanikiwa. 4Waovu hawako hivyo, wao badala yake ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. 6Kwa kuwa Yahweh huikubali njia ya wenye haki, njia ya waovu itaangamizwa.

Injili

Lk 18:35–43

35Ikawa Yesu ulipokaribia Yeriko, mtu mmoja kipofu alikuwa ameketi kando ya barabara akiomba msaada, 36aliposikia umati wa watu ukipita aliuliza nini kinatokea. 37Wakamwambia kwamba Yesu wa Nazareti anapita. 38Hivyo yule kipofu akalia kwa sauti, akisema, 'Yesu, Mwana wa Daudi, unirehemu.' 39wale waliokuwa wakitembea walimkemea huyo kipofu, wakamwambia anyamaze. Lakini yeye akazidi kulia kwa sauti, 'Mwana wa Daudi, unirehemu. 40Yesu akasimama akaamuru mtu yule aletwe kwake. Kisha yule kipofu alipomkaribia, Yesu akamwuliza, 41'Unataka nikufanyie nini?' Akasema, 'Bwana, nataka kuona.' 42Yesu akamwambia, 'Upate kuona. Imani yako imekuponya. ' 43Mara hiyo akapata kuona, akamfuata Yesu akimtukuza Mungu. Walipoona hili, watu wote wakamsifu Mungu.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 16 Novemba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki