Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 16 Novemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 3 Novemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 16 Novemba 2026
Jumatatu · Wiki ya 25 baada ya Pentekoste · Sauti ya 7
Sikukuu na watakatifu
Wafiadini Akepsimo, askofu, Yusufu, padri, na Aithala, shemasi (karne ya 4)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
1Paulo, Silwano, na Timotheo, kwa kanisa la Wathesalonike katika Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo. 2Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo. 3Imetupasa sisi kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu. Maana hivi ndivyo itupasavyo, kwa kuwa imani yenu inakua sana, na upendo wenu kwa kila mtu uongezeke mwingi. 4Hivyo sisi wenyewe tunaongea kwa fahari juu yenu katika makanisa ya Mungu. Tunazungumza habari ya saburi yenu na imani mliyo nayo katika mateso yote. Tunaongea kwa habari ya mateso mnayostahimili. 5Hii ndiyo ishara ya hukumu ya haki ya Mungu. Matokeo ya haya ni kuwa ninyi mhesabiwe kuwa mwastahili kuuingia ufalme wa Mungu ambao kwa ajili yake mnateswa. 6Kwa kuwa ni haki kwa Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi, 7na kuwapa raha ninyi mteswao pamoja nasi. Atafanya hivi wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake. 8Katika mwali wa moto atawalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu na wao wasioitii injili ya Bwana wetu Yesu. 9Watateseka kwa maangamizi ya milele wakiwa wametengwa na uwepo wa Bwana na utukufu wa nguvu zake. 10Atafanya wakati atakapokuja ili kutukuzwa na watu wake na kustaajabishwa na wote walioamini. Kwa sababu ushuhuda wetu kwenu ulisadikiwa kwenu.
Injili
29Wakati umati wa watu wanakusanyika na kuongezeka, Yesu akaanza kusema “ Kizazi hiki ni kizazi cha uovu. Hutafuta ishara, na hakuna ishara watayopewa zaidi ya ile ishara ya Yona. 30Maana kama Yona alivyokuwa ishara kwa watu wa Ninawi, ndivyo na Mwana wa Adamu atakavyokuwa ishara kwa kizazi hiki 31Malkia wa Kusini atasimama siku ya hukumu na watu wa kizazi hiki na kuwahukumu wao, kwani yeye alitoka katika mwisho wa nchi ili aje asikilize hekima za Solomoni, na hapa yuko aliye mkuu kuliko Solomoni. 32Watu wa Ninawi watasimama katika hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki siku ya hukumu watakihukumu, kwani wao walitubu kwa mahubiri ya Yona, na tazama, hapa yuko aliye mkuu kuliko Yona. 33Hakuna Mtu yeyote, awashaye taa na kuiweka sehemu ya chini yenye giza isiyoonekana au chini ya kikapu, ila huwasha na kuweka juu ya kitu ili kila mtu aingiaye aweze kuona mwanga.
Watakatifu wa siku
- Kuwekwa wakfu kwa kanisa la Mfiadini Mkuu Georgi huko Lida (karne ya 4)
- Wafiadini wa Kikasisi Basili, Petro, Basili, Aleksanda, Vladimir, Sergio, Nikolao, Vikenti, Yohana, Petro, Aleksanda, Paulo, Kosma, mapadri, na Simeoni, shemasi (1937)
- Mfiadini Eudokia (1938)
- Mfiadini wa Kikasisi Sergio, shemasi (1942)
- Wafiadini Atiko, Agapio, Eudoksio, Katerio, Istukario, Paktobio, Niktopolioni na wenzao (karibu 320)
- Mtakatifu Mtawa Akepsimo (karne ya 4)
- Mwenye Haki Snandulia (karne ya 4)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 3 Novemba katika kalenda ya kanisa ni 16 Novemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki