Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 10 Novemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 10 Novemba 2026
Jumanne · Juma la 32 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumanne ya Juma la 32 la Mwaka
Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe
Mt. Leo Mkuu, papa na mwalimu wa Kanisa · Kumbukumbu
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1Lakini wewe yaseme yale yanayoendana na maelekezo ya kuaminika. 2Wazee wawe na kiasi, heshima, busara, imani safi, katika upendo, na katika uvumilivu. 3Vilevile wanawake wazee lazima daima wajioneshe wao wenyewe kama wenye kujiheshimu, na sio wasengenyaji. Lazima wasiwe watumwa wa pombe. 4Wanapaswa kufundisha yaliyo mazuri ili kuwaandaa wasichana kwa busara kuwapenda waume zao na watoto wao. 5Wanapaswa kuwafundisha kuwa na busara, wasafi, watunzaji wazuri wa nyumba zao, na watii kwa waume zao wenyewe. Inawalazimu kufanya mambo haya ili kwamba neno la Mungu lisitukanwe. 6katika namna iyo hiyo, watieni moyo vijana wa kiume wawe na busara. 7Katika njia zote jiwekeni wenyewe kuwa mfano katika kazi nzuri; na mfundishapo, onesheni uadilifu na heshima. 8Ongeeni ujumbe wenye afya na usio na dosari, ili kwamba yeyote apingaye aaibishwe kwa sababu hana baya la kusema juu yetu. 11Kwa kuwa neema ya Mungu imeonekana kwa watu wote. 12Inatufundisha kukataa mambo yasiyo ya kimungu na tamaa za kidunia. Inatufundisha kuishi kwa busara, kwa haki, na katika njia za kimungu kwa wakati huu. 13Wakati tunatarajia kupokea tumaini letu lenye baraka, mwonekano wa utukufu wa Mungu wetu mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo. 14Yesu alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu ili kutukomboa kutoka katika uasi na kutufanya wasafi, kwa ajili yake, watu maalumu walio na hamu ya kufanya kazi nzuri.
Wimbo wa katikati
3Uwamini Mungu na kufanya yaliyo mema; uishi katika nchi na uongezeke katika imani. 4Kisha ufurahi mwenyewe katika Yahwe, naye atakupa matamanio ya moyo wako. 18Yahwe huwalinda watu wasio na lawama siku hadi siku, na urithi wao utakuwa wa milele. 23Hatua za mwanadamu zinaimarishwa na Yahwe, mtu ambaye njia zake zinakubalika machoni pa Mungu. 27Acha uovu na ufanye yaliyo mema; ndipo utakapokuwa salama milele. 29Wenye haki watairithi nchi na kuaa huko milele.
Injili
7Lakini nani miongoni mwenu, ambaye ana mtumishi anayelima shamba au anayechunga kondoo, atamwambia arudipo shambani, 'Njoo haraka na keti ule chakula? 8Je hatamwambia, 'Niandalie chakula nile, na jifunge mkanda na unitumikie mpaka nitakapo maliza kula na kunywa. Baada ya hapo uta kula na kunywa? 9Hata mshukuru mtumishi huyo kwasababu katimiza yale aliyoamriwa? 10Vivyo hivyo nanyi mkiisha kufanya mliyoagizwa semeni 'Sisi tu watumishi tusiostahili. Tumefanya tu yale tuliyopaswa kufanya.'
Watakatifu wa siku
- Mt. Leo Mkuu, papa na mwalimu wa Kanisa
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki