Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 6 Novemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 24 Oktoba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 6 Novemba 2026
Ijumaa · Wiki ya 23 baada ya Pentekoste · Sauti ya 5
Sikukuu na watakatifu
Mfiadini Aretha na pamoja naye wafiadini 4299 († 523)
Siku ya mfungo
Mfungo: pamoja na mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
14Kwa hivyo ninyi, ndugu, muwe watu wa kuiga makanisa ya Mungu yaliyoko katika Uyahudi katika Kristo Yesu. Kwa kuwa ninyi pia mliteseka katika mambo yale yale kutoka kwa watu wenu, kama ilivyo kuwa kutoka kwa wayahudi. 15walikuwa ni Wayahudi ndiyo waliomuua Bwana Yesu pamoja na manabii. Ni Wayahudi ambao walitufukuza tutoke nje. Hawampendezi Mungu na ni maadui kwa watu wote. 16Walituzuia tusiseme na Mataifa ili wapate kuokolewa. Matokeo yake ni kwamba wanaendelea na dhambi zao. Mwisho ghadhabu imekuja juu yao. 17Sisi, ndugu, tulikuwa tumetengana nanyi kwa muda mfupi, kimwili, si katika roho. Tulifanya kwa uwezo wetu na kwa shauku kuu kuona nyuso zenu. 18Kwa kuwa tulitaka kuja kwenu, mimi Paulo, kwa mara moja na mara nyingine, lakini shetani alituzuia. 19Kwa kuwa kujiamini kwetu ni nini kwa baadaye, au furaha, au taji ya kujivunia mbele za Bwana wetu Yesu wakati wa kuja kwake? Je si ninyi zaidi kama walivyo wengine?
Injili
1Baada ya mambo hayo, Bwana akachagua sabini wengine, na kuwatuma wawili wawili wamtangulie katika kila mji na eneo alilotarajia kwenda. 2Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini wafanyakazi ni wachache. Hivyo basi muombeni Bwana wa mavuno, ili kwamba atume haraka wafanyakazi katika mavuno yake. 3Enendeni katika miji. Angalieni, ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. 4Msibebe mfuko wa pesa, wala mikoba ya wasafiri, wala viatu, wala msimsalimie yeyote njiani. 5Katika nyumba yeyote mtakayo ingia, kwanza semeni, 'Amani iwe katika nyumba hii.' 6kama mtu wa amani yupo pale, amani yenu itabaki juu yake, lakini kama sivyo, itarudi kwenu. 7Bakini katika nyumba hiyo, kuleni na mnywe watakachokitoa, kwa maana mfanyakazi anastahili mshahara wake. Msihame kutoka nyumba hii kwenda nyingine. 8Mji wowote muuingiao, na wakawapokea, kuleni chochote kitakachowekwa mbele yenu, 9na ponyeni wagonjwa waliomo humo. Semeni kwao, 'Ufalme wa Mungu umekuja karibu yanu' 10Lakini katika mji wowote mtakaoingia, na wasiwapokee, nendeni nje katika barabara na semeni, 11'Hata vumbi katika mji wenu lililonata miguu mwetu tunalikung'uta dhidi yenu! Lakini tambueni hili, Ufalme wa Mungu umekaribia.' 12Ninawambieni kwamba siku ya hukumu itakuwa ni usitahamilivu zaidi kwa Sodoma kuliko mji huo. 13Ole kwako Korazini, Ole kwako Bethsaida! Kama kazi kuu zilizo fanyika ndani yako ingalifanyika Tiro na Sidoni, Wangelitubu zamani sana, wakikaa ndani ya nguo za gunia na majivu. 14Lakini itakuwa usitahamilivu zaidi siku ya hukumu kwa Tiro na Sidoni zaidi yenu. 15Wewe Kapernaumu, Unafikiri utainuliwa mpaka Mbinguni? Hapana, utashushwa chini mpaka kuzimu
Watakatifu wa siku
- Ikoni ya Mama wa Mungu iitwayo “Furaha ya Wote Wenye Huzuni” (1688)
- Mtakatifu Mtawa Zosima (1833)
- Wafiadini wa Kikasisi Laurenti, Askofu wa Balakhna, Aleksi, padri, na Mfiadini Aleksi (1918)
- Mtakatifu Mtawa Aretha Mwungamaji (1932)
- Wafiadini wa Kikasisi Yohana na Nikolao, mapadri (1937)
- Mfiadini wa Kikasisi Petro, padri (1938)
- Mbarikiwa Elesboa (Kalebu), mfalme wa Ethiopia (553-555)
- Mfiadini Sinkletika na binti zake wawili (karne ya 6)
- Watakatifu Watawa Aretha (karne ya 12), Sisoe (karne ya 13) na Theofilo (karne ya 12-13), watawa wa faragha wa Mapango ya Kyiv
- Askofu Mtakatifu Athanasio, Patriarki wa Konstantinopoli (baada ya 1311)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 24 Oktoba katika kalenda ya kanisa ni 6 Novemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki