Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 5 Novemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 23 Oktoba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 5 Novemba 2026
Alhamisi · Wiki ya 23 baada ya Pentekoste · Sauti ya 5
Sikukuu na watakatifu
Mtume Yakobo, ndugu wa Bwana kwa jinsi ya mwili (karibu 63)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
9Kwa kuwa ndugu, mnakumbuka kazi na taabu yetu. Usiku na mchana tulikuwa tukifanya kazi kusudi tusije tukamlemea yeyote. Wakati huo, tuliwahubiria injili ya Mungu. 10Ninyi ni mashahidi, na Mungu pia, ni kwa utakatifu wa namna gani, haki, na bila lawama tulivyoenenda wenyewe mbele yenu mnaoamini. 11Vivyo hivyo, mnajua ni kwa namna gani kwa kila mmoja wenu, kama baba alivyo kwa wanawe tulivyowahimiza na kuwatia moyo. Tulishuhudia 12kwamba mlipaswa kuenenda kama ulivyo mwito wenu kwa Mungu, aliyewaita kwenye ufalme na utukufu wake. 13Kwa sababu hiyo twamshukuru Mungu pia kila wakati. Kwa kuwa wakati mlipo pokea kutoka kwetu ujumbe wa Mungu mliosikia, mlipokea si kama neno la wanadamu. Badala yake, mlipokea kama kweli ilivyo, neno la Mungu. Ni neno hili ambalo linalofanya kazi kati yenu mnaoamini. 14Kwa hivyo ninyi, ndugu, muwe watu wa kuiga makanisa ya Mungu yaliyoko katika Uyahudi katika Kristo Yesu. Kwa kuwa ninyi pia mliteseka katika mambo yale yale kutoka kwa watu wenu, kama ilivyo kuwa kutoka kwa wayahudi.
Waraka (Mt. Yakobo)
11Ndugu, ninataka ninyi mjue kwamba injili niliyoitangaza haitokani na wanadamu. 12Sikuipokea kutoka kwa mtu, wala sikufundishwa. Badala yake, ilikuwa ni kwa ufunuo wa Yesu Kristo kwangu. 13Mmekwisha sikia juu ya maisha yangu ya nyuma katika dini ya Kiyahudi, jinsi nilivyokuwa nikilitesa kwa ukali kanisa la Mungu zaidi ya kipimo na kuliteketeza. 14Nilikuwa nimeendelea katika Dini ya Kiyahudi zaidi ya ndugu zangu wengi Wayahudi. Nilikuwa na bidii sana katika tamaduni za baba zangu. 15Lakini Mungu alipendezwa kunichagua mimi kutoka tumboni mwa mama. Aliniita mimi kupitia neema yake 16kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili kwamba nimtangaze yeye miongoni mwa watu wa mataifa. Wala sikutafuta ushauri wa mwili na damu 17na sikupanda kwenda Yerusalem kwa wale waliokuwa mitume kabla yangu. Badala yake nilienda Uarabuni na baadae kurudi Damesiki. 18Kisha baada ya miaka mitatu nilipanda kwenda Yerusalemu kumtembelea Kefa, nikakaa naye kwa siku kumi na tano. 19Lakini sikuona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndungu yake na Bwana.
Injili
49Yohana akajibu akasema, “Bwana, tulimuona mtu akifukuza pepo kwa jina lako na tukamzuia, kwa sababu haambatani na sisi.” 50Lakini Yesu akamwambia, “Msimzuie, kwa kuwa asiye kinyume na ninyi ni wa kwenu” 51Ikatokea kwamba, kulinga na siku zilivyokua zikikaribia zsiku zake za kwenda mbinguni, kwa uimara alielekeza uso wake Yerusalemu. 52Akatuma wajumbe mbele yake, nao wakaenda na kuingia katika kijiji cha Wasamaria ili wamtayarishie mahali. 53Lakini watu huko hawakumpokea, kwasababu alikua ameelekeza uso wake Yerusalemu. 54Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipo liona hili, wakasema, “Bwana unahitaji tuamuru moto ushuke chini kutoka mbinguni uwateketeze?” 55Lakini aliwageukia akawakemea. 56Kisha walikwenda kijiji kingine.
Injili (Mt. Yakobo)
54Kisha Yesu akafika katika mkoa wake na akawafundisha watu katika sinagogi. Matokeo yake ni kuwa walishangaa na kusema, “Ni wapi mtu huyu alipopata hekima hii na miujiza hii? 55Mtu huyu siyo mwana wa seremala? Mariamu siyo mamaye? Na ndugu zake siyo Yakobo, Yusuph, Simoni na Yuda? 56Na dada zake tunao hapa petu? Basi mtu huyu ameyapata wapi haya yote?”. 57Aliwachukiza. Lakini Yesu aliwambia, “Nabii hakosi kuwa na heshima isipokuwa kwao na katika nchi yao. 58Na hakuweza kufanya miujiza mingi kwa sababu hawakuwa na imani naye.
Watakatifu wa siku
- Wafiadini wa Kikasisi Nikolao, Vladimir, Aleksanda, Nikolao, Emiliani na Sozonti, mapadri (1937)
- Mtawa Mfiadini Eufrosini (1942)
- Askofu Mtakatifu Ignatio, Patriarki wa Konstantinopoli (877-878)
- Mtakatifu Mtawa Elisha wa Lavryshev (karibu 1250)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 23 Oktoba katika kalenda ya kanisa ni 5 Novemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki