Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 6 Novemba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 6 Novemba 2026

Ijumaa · Juma la 31 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Ijumaa ya Juma la 31 la Mwaka

Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: kijani

Kufunga na toba

Siku ya toba

Kila Ijumaa ni siku ya toba; kila baraza la maaskofu huamua jinsi inavyoadhimishwa: kujinyima nyama au tendo lingine la toba. Kufunga kunawahusu wenye miaka 18 hadi 59, kujinyima nyama kuanzia miaka 14.

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Flp 3:17–4:1

17Ndugu zangu, niigeni mimi. Waangalieni kwa makini wale wanaoenenda kwa mfano ulio wa jinsi yetu. 18Wengi wanaoishi niwale ambao mara nyingi nimewaambieni, na sasa nawaambia kwa machozi -wengi wanaishi kama maadui wa msalaba wa Kristo. 19Mwisho wao ni uharibifu. Kwa kuwa Mungu wao ni tumbo, na kiburi chao kiko katika aibu yao. Wanafikiria mambo ya kidunia. 20Bali uraia wetu uko mbinguni, ambako tunamtarajia mwokozi wetu Yesu Kristo. 21Atabadilisha miili yetu dhaifu kuwa kama mwili wake wa utukufu; kwa uweza ule ule unaomwezesha kuvidhibiti vitu vyote. 4:1Kwa hiyo wapendwa wangu, ambao nawatamani, ambao ni furaha na taji yangu. Simameni imara katika Bwana, enyi rafiki wapendwa.

Wimbo wa katikati

Zab 122:1–2, 4–5

1Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu, wa Daudi. Nilifurahi waliponiambia, “Na twende kwenye Nyumba ya Yahwe.” 2Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama ndani ya malango yako! 4Makabila huenda juu Yerusalemu, makabila ya Yahwe; kama ushuhuda wa Israeli, kulishukuru jina la Yahwe. 5Huko viliwekwa viti vya hukumu, viti vya enzi vya nyumba ya Daudi.

Injili

Lk 16:1–8

1Yesu aliwaambia tena wanafunzi wake, “Palikuwa na mtu mmoja tajiri aliyekuwa na meneja, na alitaarifiwa ya kwamba meneja huyu anatapanya mali zake. 2Hivyo tajiri akamwita, akamwambia, “Ni nini hii ninayo isikia juu yako? Toa hesabu ya umeneja wako, kwa kuwa huwezi kuwa meneja tena.' 3Yule meneja akasema moyoni mwake, Nifanye nini, maana bwana wangu ananiondolea kazi yangu ya umeneja? Sina nguvu za kulima, na kuomba naona haya. 4Najua nitakalotenda ili nitakapotolewa katika kazi yangu ya uwakili watu wanikaribishe nyumbani mwao. 5Hivyo wakili akawaita wadeni wa bwana wake kila mmoja akamwambia wa kwanza, 'unadaiwa kiasi gani na bwana wangu?' 6Akasema vipimo mia moja vya mafuta akamwambia 'chukua hati yako keti upesi andika hamsini.' 7kisha akamwambia mwingine na wewe unadaiwa kiasi gani?' akasema 'vipimo mia moja vya unga vya ngano.' Akamwambia 'twaa hati yako andika themanini.' 8Yule bwana akamsifu meneja dhalimu kwa vile alivyotenda kwa wereu. Kwakua watoto wa ulimwengu huu ni werevu nyingi na hushughulika kwa ujanja na watu wa upande wao kuliko walivyo watoto wa nuru.

Watakatifu wa 6 Novemba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki