Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2026 › 27 Oktoba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 27 Oktoba 2026
Jumanne · Juma la 30 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumanne ya Juma la 30 la Mwaka
Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: kijani
Masomo ya siku
Somo la kwanza
21Jitoeni wenyewe kila mmoja kwa mwingine kwa heshima ya Kristo. 22Wake, jitoeni kwa waume zenu, kama kwa Bwana. 23Kwa sababu mume ni kichwa cha mke, kama Kristo alivyo kichwa cha kanisa. Ni mwokozi wa mwili. 24Lakini kama kanisa lilivyo chini ya Kristo, vilevile wake lazima wafanye hivyo kwa waume zao katika kila jambo. 25Waume, wapendeni wake zenu kama vile Kristo alivyolipenda kanisa na akajitoa mwenyewe kwa ajili yake. 26Alifanya hivyo ili liwe takatifu. Alilitakasa kwa kuliosha na maji katika neno. 27Alifanya hivi ili kwamba aweze kujiwasilishia mwenyewe kanisa tukufu, pasipo na doa wala waa au kitu kifananacho na haya, badala yake ni takatifu lisilo na kosa. 28Kwa njia ile ile, waume wanatakiwa kuwapenda wake zao kama miili yao. Yule ampendae mke wake anajipenda mwenyewe. 29Hakuna hata mmoja anayechukia mwili wake. Badala yake, huurutubisha na kuupenda, kama Kristo pia alivyolipenda kanisa. 30Kwa kuwa sisi ni washiriki wa mwili wake. 31“Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na ataungana na mke wake, na hao wawili watakuwa mwili mmoja”. 32huu ulikuwa umefichika. Lakini ninasema kuhusu Kristo na kanisa. 33Walakini, kila mmoja wenu lazima ampende mke wake kama mwenyewe, na mke lazima amheshimu mumewe.
Wimbo wa katikati
1Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu. Amebarikiwa kila mtu amchaye Yahwe, atembeaye katika njia zake. 2Kazi ya mikono yako, wewe utaifurahia; utabarikiwa na kufanikiwa. 3Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao katika nyumba yako; wanao watakuwa kama miche ya mimea ya mizeituni wakaapo kuzunguka meza yako. 4Ndiyo, hakika, mtu anaye muheshimu Yahwe atabarikiwa. 5Mungu na akubariki toka Sayuni; na uweze kuona mafanikio ya Yerusalemu siku zote za maisha yako.
Injili
18Yesu akasema, “Ufalme wa Mungu unafanana na nini, na naweza kuulinganisha na nini? 19Ni kama mbegu ya haradari aliyoitwaa mtu mmoja na kuipanda shambani mwake, na ikamea ikawa mti mkubwa, na ndege wa mbinguni wakajenga viota vyao katika matawi yake. 20Tena akasema, “Niufananishe na nini ufalme wa Mungu? 21Ni kama chachu ambayo mwanamke aliichukua na kuchanganyakwenye vipimo vitatu vya unga hata ukaumuka.”
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki