Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2026 › 23 Oktoba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 23 Oktoba 2026

Ijumaa · Juma la 29 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Ijumaa ya Juma la 29 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Mt. Yohane wa Kapistrano, padre · Kumbukumbu ya hiari

Kufunga na toba

Siku ya toba

Kila Ijumaa ni siku ya toba; kila baraza la maaskofu huamua jinsi inavyoadhimishwa: kujinyima nyama au tendo lingine la toba. Kufunga kunawahusu wenye miaka 18 hadi 59, kujinyima nyama kuanzia miaka 14.

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Efe 4:1–6

1Kwa hiyo, kama mfungwa kwa ajili ya Bwana, nawasihi mtembee sawasawa na wito ambao Mungu aliwaita. 2Muishi kwa unyenyekevu mkuu na upole na uvumilivu. Mkichukuliana katika upendo. 3Fanyeni bidii kuutunza umoja wa Roho katika kifungo cha amani. 4Kuna mwili mmoja na Roho moja, kama ambavyo pia mlikuwa mmeitwa katika uhakika wa taraja moja la wito wenu. 5Na kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja, 6na Mungu mmoja na Baba wa wote. Yeye yuko juu ya yote, na katika yote na ndani ya yote.

Wimbo wa katikati

Zab 24:1–6

1Zaburi ya Daudi. Nchi ni ya Yahwe, na vyote viijazavyo, dunia, na wote wakaao ndani yake. 2Kwa kuwa yeye aliianzisha juu ya bahari na kuiimarisha juu ya mito. 3Ni nani atakaye panda mlima wa Yahwe? Ni nani atakaye simama patakatifu pake? 4Yeye ambaye ana mikono misafi na moyo safi; ambaye hajauinua uongo, na haja apa kiapo ili kudanganya. 5Yeye atapokea baraka kutoka kwa Yahwe na haki kutoka kwa Mungu wa wokovu wake. 6Kizazi cha wale wamtafutao Mungu ni kama hiki, wale ambao wanautafuta uso wa Mungu wa Yakobo.

Injili

Lk 12:54–59

54Yesu akawa anawaambia makutano pia, “Mara muonapo mawingu yakitokea magharibi, mnasema nyakati za mvua zimewadia; na ndivyo inavyo kuwa, 55Na upepo wa kusini ukivuma, mnasema, Patakuwepo na joto kali, na ndivyo inavyokuwa. 56Enyi wanafiki, mnaweza kutafsiri mwonekano wa nchi na anga, lakini inakuwaje hamuwezi kuutafsiri wakati uliopo? 57Ni kwa nini kila mmoja wenu asipambanue lililo sahihi kwake kulifanya wakati ambapo angali na nafasi ya kufanya hivyo? 58Maana mkienda na mshitaki wako mbele ya hakimu, jitahidi kupatana na mshitaki wako mungali bado mko njiani asije akakupeleka kwa hakimu, na hakimu akupeleka kwa ofisa, na ofisa akakutupa gerezani. 59Nakuambia, hutatoka huko hadi umelipa mpaka senti ya mwisho.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 23 Oktoba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki