Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2026 › 22 Oktoba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 22 Oktoba 2026

Alhamisi · Juma la 29 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Alhamisi ya Juma la 29 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Mt. Yohane Paulo II, papa · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Efe 3:14–21

14Kwa sababu hii napiga magoti kwa Baba. 15ambaye kwa yeye kila familia mbinguni na juu ya nchi imeitwa jina. 16Ninaomba kwamba apate kuwanemesha, kutokana na utajiri wa utukufu wake, awafanye imara kwa nguvu kupitia Roho wake, ambaye yu ndani yenu. 17Ninaomba kwamba Kristo aishi ndani ya mioyo yenu kupitia imani. 18Ninaomba kwamba muwe na shina na msingi wa upendo wake. Muwe katika pendo lake ili muweze kuelewa, pamoja na wote waaminio, jinsi upana, na urefu na kimo na kina cha upendo wa Kristo. 19Ninaomba Kwamba mjue ukuu wa upendo wa Kristo, ambao unazidi ufahamu. Mfanye haya ili mjazwe na ukamilifu wote wa Mungu. 20Na sasa kwake yeye awezaye kufanya kila jambo, zaidi ya yote tuyaombayo au tuyawazayo, kupitia nguvu yake itendayo kazi ndani yetu, 21kwake yeye kuwe utukufu ndani ya kanisa na katika Kristo Yesu kwa vizazi vyote milele na milele. Amina.

Wimbo wa katikati

Zab 33:1–2, 4–5, 11–12, 18–19

1Furahini katika Yahwe, ninyi wenye haki; kusifu kwa wenye haki kwa faa sana. 2Mshukuruni Bwana kwa kinubi; mwimbieni sifa kwa kinubi chenye nyuzi kumi. 4Kwa kuwa maneno ya Mungu ni ya hakika, na kila afanyacho ni haki. 5Yeye hupenda haki na kutenda kwa haki. Dunia imejaa uaminifu wa agano la Yahwe. 11Mipango ya Yahwe husimama milele, mipango ya moyo wake ni kwa ajili ya vizazi vyote. 12Limebarikiwa taifa ambalo Mungu wao ni Yahwe, watu ambao yeye amewachagua kama warithi wake. 18Tazama, macho ya Yahwe yako kwa wale wanao mhofu yeye, wale wanao litumainia agano lake takatifu 19kuwaokoa maisha yao na mauti na kuwaweka hai wakati wa jaa.

Injili

Lk 12:49–53

49Nimekuja kuwasha moto duniani, na natamani iwe umekwishawaka, 50Lakini nina ubatizo ambao nitabatizwa, na nina huzuni mpaka utkapokamilika! 51Je mnafikiri kuwa nimekuja kuleta amani duniani? Hapana, Nawaambieni, badala yake nimeleta mgawanyiko. 52Tangu sasa na kuendelea kutakuwa na watu watano katika nyumba moja wamegawanyika, na watatu watakuwa kinyume na wawili, na wawili watakuwa kinyume na watatu. 53Watagawanyika, baba atakuwa kinyume na mwanae, na mwanae atakuwa kinyume na babaye, mama atakuwa kinyume na binti yake, na binti atakuwa kinyume na mama yake, Mama mkwe atakuwa kinyume na mkwe wake naye mkwe atakuwa kinyume na mama mkwe wake.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 22 Oktoba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki