Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2026 › 11 Oktoba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 11 Oktoba 2026
Jumapili · Juma la 28 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Dominika ya 28 ya Mwaka
Dominika · Rangi ya liturujia: kijani
Masomo ya siku
Somo la kwanza
6Katika mlima huu Yahwe wa majeshi atafanya kwa watu sikukuu ya ya vitu vilivyonona, na mvinyo uliochaguliwa, zabuni ya nyama na sikuku juu ya sira. 7Na katika mlima huu atauharibu mfuniko uliowekwa juu watu wote, na mtandao wa kusuka juu ya mataifa. 8Atameza kifo daima, na Bwana Yahwe atayafuta machozi katika nyuso zetu; na aibu ya watu wake itatupwa mbali kutoka duniani kote, maana Yahwe amesema hivyo. 9Yatazungumzwa katika siku hiyo, ''Huyu ni Mungu wetu; na tunayemngoja, na atatuokoa. Huyu ni Yahwe; tuliyemngoja, tutafurahia na kushangilia wokovu wake.'' 10Maana katika mlima huu mkono wa Bwana utashuka; na Moabu itakanyagwakangwa chini kwenye eneo lake, na hata majani yatakanyagwakanyagwa chini katika shimo lililojaa mbolea.
Wimbo wa katikati
1Zaburi ya Daudi. Yahwe ni mchungaji wangu; sita pungukiwa na kitu. 2Yeye hunilaza katika majani mabichi; huniongoza kando ya maji matulivu. 3Yeye huurejesha uhai wangu; huniongoza katika njia iliyo sahihi kwa ajili ya jina lake. 4Hata ijapokuwa nikipita katika bonde la uvuli na giza nene, sitaogopa kudhurika kwa kuwa wewe uko pamoja nami; fimbo yako na gongo lako vya nifariji. 5Wewe waandaa meza mbele yangu katika uwepo wa maadui zangu; umenipaka mafuta kichwa changu na kikombe changu kinafurika. 6Hakika wema na uaminifu wa agano vitaniandama siku zote za maisha yangu; nami nitaishi katika nyumba ya Yahwe milele!
Somo la pili
12Nafahamu kuishi katika hali ya kupungukiwa na pia katika hali ya kuwa na vingi. Katika mazingira yote haya mimi nimejifunza siri ya namna ya kula wakati wa shibe na jinsi ya kula wakati wa njaa, yaani vingi na kuwa mhihtaji. 13Ninaweza kufanya haya kwa kuwezeshwa na Yeye anitiaye nguvu. 14Hata hivyo, mlifanya vyema kushiriki nami katika dhiki zangu. 19Kwa ajili hiyo, Mungu wangu atawajazeni mahitaji yenu kwa utajiri wa utukufu wake katikaYesu Kristo. 20Sasa kwa Mungu na Baba yetu uwe utukufu milele na milele. Amina.
Injili
1Yesu alisema nao tena katika mifano, akisema, 2“Ufalme wa mbinguni unafanana na mfalme aliyeandaa sherehe ya harusi ya mwanawe. 3Akawatuma watumishi wake kuwakaribisha waliokuwa wamealikwa kuja katika sherehe ya harusi, lakini hawakufika. 4Mfalme aliwatuma tena watumishi wengine, akisema. “Waambieni wote walioalikwa, Angalieni, nimeandaa chakula. Fahali na ndama wangu wanono wamechinjwa, na mambo yote yako tayari, Njoni katika sherehe ya harusi.” 5Lakini watu hao hawakuzingatia kwa dhati mwaliko wake. Baadhi walirejea katika mashamba yao, na wengine walirudi katika sehemu zao za biashara. 6Wengine waliwainukia watumishi wa mfalme na kuwadharirisha na kuwaua. 7Lakini mfalme alikasirika. Alituma jeshi lake, akawaua wale wauaji na kuuteketeza mji wao kwa moto. 8Kisha aliwaambia watumishi wake, “Harusi iko tayari, lakini walioalikwa hawakustahili. 9Kwa hiyo nendeni kwenye makutano ya njia kuu, waalikeni watu wengi kadri iwezekanavyo waje kwenye sherehe ya harusi.” 10Watumishi walienda njia kuu na kuwakaribisha watu wowote waliowaona, wema na wabaya. Hivyo ukumbi wa harusi ulijaa wageni. 11Lakini mfalme alipoingia kuwatazama wageni, alimuona mtu mmoja ambaye hakuvaa vazi rasmi la harusi! 12Mfalme alimwuliza, 'Rafiki, ulipataje kufika hapa ndani bila vazi la harusi?' Na mtu huyo hakujibu chochote. 13Ndipo mfalme alipowaambia watumishi wake, “Mfungeni mtu huyu mikono na miguu na mtupeni nje katika giza, huko ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno. 14Kwa kuwa watu wengi wanaitwa, lakini wateule ni wachache.”
Watakatifu wa siku
- Mt. Yohane XXIII, papa
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki