Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2026 › 8 Oktoba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 25 Septemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 8 Oktoba 2026
Alhamisi · Wiki ya 19 baada ya Pentekoste · Sauti ya 1
Sikukuu na watakatifu
Mtakatifu Mtawa Eufrosini wa Aleksandria (karne ya 5)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Sala ya Jioni: somo
31Katika kinywa cha wale watendao haki hutoka tunda la hekima, bali ulimi wa kupotosha utakatwa. 32Midomo ya wale watendao mema huyajua yanayokubalika, bali kinywa cha waovu, huyajua yanayopotosha. 11:1Yehova huchukia vipimo ambavyo havipo sahihi, bali hufurahia uzani dhahiri. 2Kinapokuja kiburi, ndipo aibu huja, bali unyenyekevu huleta hekima. 3Uadilifu wa wenye haki huwaongoza, bali udanganyifu wa njia za wajanja utawaangamiza. 4Utajiri hauna thamani siku ya ghadhabu, bali kwa kutenda haki hujilinda na mauti. 5Mwenendo wa mtu mwema huinyosha njia yake, bali waovu wataanguka kwa sababu ya uovu wao. 6Mwenendo mwema wa wale wampendezao Mungu utawalinda salama, bali wadanganyifu hunaswa katika shauku zao. 7Mtu mwovu anapokufa, tumaini lake hupotea na tumaini lililokuwa katika nguvu zake linakuwa si kitu. 8Yule atendaye haki hulindwa katika taabu na badala yake taabu humjia mwovu. 9Kwa kinywa chake asiyeamini Mungu humwangamiza jirani yake, bali kwa maarifa wale watendao haki hulindwa salama. 10Wanapofanikiwa watendao haki, mji hufurahi, waovu wanapoangamia, kunakuwa na kelele za furaha. 11Kwa zawadi nzuri za wale wanaompendeza Mungu, mji unakuwa mkubwa; kwa kinywa cha waovu mji huvurugwa. 12Mtu mwenye dharau kwa rafiki yake hana akili, bali mtu mwenye ufahamu hunyamaza.
Sala ya Jioni: somo
Haimo katika tafsiri hii
Sala ya Alfajiri: Injili
27Mambo yote yamekabidhiwa kwangu kutoka kwa Baba. Na hakuna amjuaye Mwana isipokuwa Baba, na hakuna amjuaye Baba isipokuwa Mwana, na yeyote ambaye Mwana ana hamu ya kumfunulia. 28Njoni kwangu, nyinyi nyote mnaosumbuka na mnaolemewa na mzigo mzito, nami nitawapumzisha. 29Jitieni nira yangu na mjifunze kutoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mnyenyekevu na mpole wa moyo na mtapata pumziko la nafsi zenu. 30Kwa kuwa nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.
Waraka (Mt. Sergio)
22Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, ukarimu, utu wema, imani, 23upole, na kiasi. Hakuna sheria dhidi ya mambo kama hayo. 24Wale walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na shauku na tamaa zao mbaya. 25Kama tukiishi kwa Roho, pia tutembee kwa Roho. 26Tusiwe wa kujivuna, tusichokozane kila mmoja na mwenzake, wala tusioneane wivu. 6:1Ndugu, ikiwa mtu amekamatwa katika uovu, ninyi mlio wa kiroho, mnawiwa kumrejesha huyo ndugu katika roho ya upole. Huku mkijiangalia wenyewe ili msijaribiwe. 2Mchukuliane mizigo, na kwa hiyo mtaikamilisha sheria ya Kristo.
Injili (Mt. Sergio)
17Kisha Yesu alitelemka pamoja nao toka mlimani na kusimama mahali tambarare. Idadi kubwa ya wanafunzi wake walikuwa huko, pamoja na idadi kubwa ya watu kutoka Uyahudi na Yerusalemu, na kutoka pwani ya Tiro na Sidoni. 18Walikuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. Watu waliokuwa wakisumbuliwa na pepo wachafu waliponywa pia. 19Kila mmoja kwenye hilo kusanyiko alijaribu kumgusa kwa sababu nguvu za uponyaji zilikuwa zikitokea ndani yake, na aliwaponya wote. 20Kisha akawaangalia wanafunzi wake, na kusema, “Mmebarikiwa ninyi mlio maskini, kwa maana ufalme wa Mungu ni wenu. 21Mmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa, kwa maana mtashibishwa. Mmebarikiwa ninyi mliao sasa, kwa maana mtacheka. 22Mmebarikiwa ninyi ambao watu watakapowachukia na kuwatenga na kuwashutumu ninyi kwamba ni waovu, kwa ajili ya Mwana Adamu. 23Furahini katika siku hiyo na kurukaruka kwa furaha, kwa sababu hakika mtakuwa na thawabu kubwa mbinguni, kwa maana baba zao waliwatendea vivyohivyo manabii.
Watakatifu wa siku
- Kufariki kwa Mtakatifu Mtawa Sergio, abati wa Radonezh, mtenda miujiza wa Urusi yote (1392)
- Mtakatifu Nikolao Mwungamaji, padri (1941)
- Mtawa Mfiadini Pafnuti Mmisri na pamoja naye wafiadini 546 (karne ya 3)
- Mtakatifu Mtawa Eufrosini wa Suzdal, aliyeitwa Theodulia duniani (1250)
- Kuhamishwa kwa masalia ya Askofu Mtakatifu Germano, Askofu Mkuu wa Kazan (1595)
- Mtakatifu Mtawa Dositheya, mtawa wa faragha, wa Kyiv (1776)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 25 Septemba katika kalenda ya kanisa ni 8 Oktoba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki