Bible Explorer

Gundua › Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando › Kutoka Hezekia hadi Yosia

Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando · Kutoka Hezekia hadi Yosia

Pasaka ya Yosia

2 Fal 23:21–23 · 2 Nya 35:1–19

2 Wafalme

2 Fal 23:21–23

21Kisha mfalme akawaamuru watu wote, akisema, “Itunzeni Pasaka ya Yahwe Mungu wenu, kama ilivyoandikwa kwenye hiki kitabu cha agano.”

22Hiyo Pasaka haijawahi kufanyika tangu siku za waamuzi ambao waliiongoza Israeli, wala katika siku zote za wafalme wa Israeli au Yuda.

23Lakini katika mwaka wa kumi na nane wa Mfalme Yosia hii Pasaka ya Yahwe ilisheherekewa katika Yerusalemu.

2 Mambo ya Nyakati

2 Nya 35:1–19

1Yosia asherehekea Pasaka kwa ajili ya Yahwe katika Yerusalemu, na wakachinja wanakondoo katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.

2Akawaweka makauhuni katika nafasi zao na akawatia moyo katika hudumza za nyumba ya Yahwe.

3Akasema kwa Walawi waliowafundisha Israeli wote na waliokuwa wamewekwa wakifu kwa Yahwe. “Liwekeni sanduka takatifu katika nyumba ambayo Selemani mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli aliijenga. Msilibebe kuzunguka nalo tena mabegani mwenu. Sasa mwabuduni Yahwe Mungu wenu, na watumikieni watu wake Israeli.

4Jikusanyeni wenyewe kwa majina ya nyumba za babu zenu na zamu zenu, mkifuata maelekezo ya Daudi, mfalme wa Israeli, na yale ya Selemani, mwaye.

5Simeni katika sehemu takatifu, mkichukua nafasi zenu kwa zamu zenu ndani ya nyumba za mababu wa bdugu zenu, uzao wa watu, na mchukue sehemu zenu kwa zamu zenu ndani ya nyumba za mababu wa Walawi.

6Chinjeni wanakondoo wa Paska, jitakaseni wenyewe, andaeni wankondoo kwa ajili ya ndugu zenu, kufanya sawa sawa na neno la Yahwe ambalo lilitolewa kwa mkono wa Musa”.

7Yosia akawapa watu wote wanakondoo elfu thelathini na wanambuzi kutoka katika makundi kwa ajili ya sadaka za Pasaka kwa wote walikuwepo. Pia akatoa ng'ombe dume elfu tatu; hawa walikuwa kutoka katika mali ya mfalame.

8Viongozi wake wakatoa sadaka za hiari kwa watu, makuhani, na Walawi. Hilki, Zekaria, na Yeieli, viongozi wasimamizi wa nyumba ya Mungu, wakawapa makuhani ndama 2,600 na maksai mia tatu kwa ajili ya matoleo ya Paska.

9Pia Konania, Shemaya na Nethaneli, ndugu zake, na Hashabia, Yeieli, na Yazabadi, mkuu wa Walawi, akawapa Walawi ndama elfu tano kwa ajili ya matoleo ya Pasaka.

10Kwa hiyo huduma iliandaliwa, na makuhani wakasimama katika sehemu zao, pamoja na Walawi kwa zamu zao, kwa mjibu wa agizo la mfalme.

11Wakawachinja wanakondoo wa Pasaka, na makuhani wakainyunyiza damu waliyoipokea kutoka kwenye mikono ya Walawi, na Walawi wakawachuna wanakondoo.

12Wakaziondoa sadaka za kuteketezwa, ili kuzisambaza katika makundi ya nyumba za mababu wa watu, ili wamtolee Yahwe, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Musa. Wakafanya vile vile kwa wale ng'ombe dume.

13Wakawaoka kwa moto wanakondoo wa Pasaka wakifuata maelekezo, kuhusu sadaka takatifu, walizichemsha kwenye vyungu, masufuria na makaangoni, na haraka wayapeleka kwa watu.

14Baadaye waliandaa sadaka kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya makuhani, kwa sababu makuhani, uzao wa Haruni, walikuwa wametingwa katika kazi ya kutoa sadaka za kuteketezwa na za mafuta hadi usiku ulipoingia, kwa hiyo Walawi wakaandaa sadaka kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya makuhani, wana wa Haruni.

15Waimbaji, wana wa Asafu, walikuwa katika nafasi zao, kama ilivyoagiwa na Daudi, Asafu, Hemani, na Yeduthuni, mwonaji wa mfalme, na walinzi walikuwa katika kila lango. Hawakutakiwa kuviacha vituo vyao, kwa sababu ndugu zao Walawi walifanya maandalizi kwa ajili yao.

16Kwa hiyo, wakati huo huduma yote ya Yahwe ilifanyika kwa ajili ya kusherekea Pasaka na kutoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya Yahwe, Kama alivyoamuru mfalme Yosia.

17Watu wa Israeli ambao walikuwepo wakaishika Sabato wakati huo, na kisha Sikukuu ya Mikate isiyochachwa kwa siku saba.

18Pasika kama hiyo haijafanyika tena katika Israeli tangu siku za nabii Samweli, wala hakuna mfalme yeyote miongoni mwa wafalme wa Israeli ambaye amewahi kusherekea Pasaka kama Yosia alivyofanya, pamoja na makuhani, Walawi, na watu wote wa Yuda na Israeli waliokuwepo, na wakaaji wote wa Yerusalemu.

19Pasaka hii ilitunzwa ndani ya miaka kumi na nane ya utawala wa Yosia.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY