Gundua › Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando › Kutoka Hezekia hadi Yosia
Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando · Kutoka Hezekia hadi Yosia
Yosia afanya upya agano
2 Fal 23:1–3 · 2 Nya 34:29–32
2 Fal 23:1–31Hivyo mfalme akawatuma wajumbe waliokuwa wamemzunguka wazee wote wa Yuda na wa Yerusalemu.
2Kisha mfalme akapanda hadi kwenye nyumba ya Yahwe, na watu wote wa Yuda na wenyeji wote wa Yerusalemu pamoja naye, na makuhani, manabii, na watu wote, kuanzia mdogo hadi mkubwa. Kisha akasoma katika masikioni kwao maneno yote ya kitabu cha agano ambalo lililokuwa limepatikana kwenye nyumba ya Yahwe.
3Mfalme akasimama karibu na nguzo na kufanya agano mbele ya Yahwe, kutembea pamoja na Yahwe na kukumbuka maagizo yake, kanuni zake, na sheria zake, kwa moyo wake wote na kwa roho yake yote, kuthibitisha maneno ya hili agano ambalo lililokuwa limeandikwa kwenye hiki kitabu. Hivyo watu wote wakakubaliana kusimama kwenye agano
2 Nya 34:29–3229Mfalme akatuma wajumbe na kuwakusanya wazee wote wa Yuda na Yerusalemu.
30Kisha mfalme akaenda kwenye nyumba ya Yahwe, na watu wote wa Yuda wakaaji wa Yerusalemu, na makuhani, Walawi, na watu wote, kuanzia wakubwa hadi wadogo. Kisha akasoma mbele zao maneno yote ya kitabu cha Agano kilichokuwa kimeokotwa katika nyumba ya Yahwe.
31Mfalme aksimama katika sehemu yake na kufanya aganao mbele za Yahwe, kutembea mbele za Yahwe, na kuzishika amri zake, taratibu zake, na sheria zake, kwa moyo wake wote na roho yake yote, kuyatii maneno ya agano yaliyokuwa yameandikwa katika agano ambayo yalikuwa yameandikwa katika kitabu hiki.
32Aliwasababisha wote walioonekana katika Yerusalemu na Benyamini kusimama kwa agano. Wakaaji wa Yerusalemu wakatembea kwa agano la Mungu, Mungu wa babu zao.
Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.
Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY