Bible Explorer

Gundua › Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando › Wafalme wa Yuda

Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando · Wafalme wa Yuda

Yehoramu mfalme wa Yuda

2 Fal 8:16–24 · 2 Nya 21:5–10

2 Wafalme

2 Fal 8:16–24

16Katika mwaka wa kumi na tano wa Yoramu mwana wa Ahabu, mfalme wa Israeli, Yehoramu akaanza kutawala. Alikuwa mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda. Alianza wakati Yehoshafati alikuwa mfalme wa Yuda.

17Yoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na mbili alipoanza kutawala, na alitawala kwa mda wa miaka minane katika Yerusalemu.

18Yoramu akatembea kwenye njia ya huyo mfalme wa Israeli, kama walivyokuwa wakifanya kwenye nyumba ya Ahabu; kwa kuwa alikuwa na binti wa Ahabu kama mke wake, na alifanya uovu usoni kwa Yahwe.

19Walakini, kwa sababu ya mtumishi wake Daudi, Yahwe hakutaka kuiharibu Yuda, tangu alipomwambia kwamba atampatia wazao.

20Katika siku za Yoramu, Edomu akaasi kutoka chini ya mkono wa Yuda, na wakamfanya mfalme juu yao wenyewe.

21Basi Yehoramu akaenda na maamri jeshi na magari ya farasi yote. Ilitokea kwamba akaamka usiku na kushambulia na kuwazunguka Waedomu, waliokuwa wamemzunguka na wale maamri jeshi wa magari ya farasi. Ndipo wanajeshi wa Yehoramu wakakimbilia wajumbani kwao.

22Hivyo Edomu aliasi dhidi ya utawala wa Yuda katika siku hizi. Libna pia aliasi katika kipindi hicho hicho.

23Kwa mambo mengine yamhusuyo Yehoramu, yote aliyoyafanya, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya mfalme wa Yuda?

24Yehoramu akafa na kuzikwa pamoja na baba zake, na akalala pamoja na baba zake katika mji wa Daudi. Ndipo Ahazi mtoto wake akawa mfalme katika sehemu yake.

2 Mambo ya Nyakati

2 Nya 21:5–10

5Yehoramu alikuwa na umri wa mika thelathini na mbili alipoanza kutawala, na akatawala kwa miaka minane katika Yerusalemu.

6Akatembea katika njia za wafalme wa Israeli, kama nyumba ya Ahabu ilivyokuwa ikifanya, kwa maana alikuwa na binti Ahabu kama mke wake, na akafanya yaliyo maovu katika macho ya Yahwe.

7Vile vile, Yahwe hakutaka kuiangamiza nyumba ya Daudi, kwa sababu ya agano ambalo alikuwa amefanya na Daudi; alikuwa ameahidi kwamba siku zote angetoa uzima kwa ajili yake na kwa ajili ya vizazi vyake.

8Katika siku za Yehoramu, Edomu wakaasi wasiwe chini ya Yuda, na wakajisimamishia mfalme juu yao.

9Kisha Yeroboamu akavuka ng'ambo pamoja na maakida na magari yake yote. Ilikuwa usiku aliposimama na kupigana dhidi ya Waedomu ambao walikuwa wamemzunguka na maakida wa magari yake.

10Kwa hiyo Edomu iliasi kutoka kuwa chini ya Yuda mpaka leo. Libna pia aliasi wakati ule ule wasiwe chini yake. Kwa sababu Yehoramu alikuwa amemsahau Yahwe, Mungu wa babu zake.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY