Bible Explorer

Gundua › Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando › Anguko la Yerusalemu

Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando · Anguko la Yerusalemu

Yehoyakimu mfalme wa Yuda

2 Fal 23:36–37; 24:1–7 · 2 Nya 36:5–8

2 Wafalme

2 Fal 23:36–37; 24:1–7

23:36Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, na alitawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa akiitwa Zebida; alikuwa binti wa Pedaia wa Ruma.

23:37Yehoyakimu akafanya yale yaliyo maovu usoni kwa Yahwe, kama waliyoyafanya babu zake.

24:1Katika siku za Yehoyakimu, Nebukadreza mfalme wa Babeli akaiteka Yuda; Yehoyakimu akawa mtumishi kwa muda wa miaka mitatu. Kisha Yehoyakimu akarudi na kuasi dhidi ya Nebukadreza.

24:2Yahwe akatuma vikosi vya Wakaldayo dhidi ya Yehoyakimu,, Washami, Wamoabu, na Waamoni; akawatuma dhidi ya Yuda kuiharibu. Hii ilikuwa ni kuthibitisha pamoja na neno la Yahwe ambalo aliloliongea kupitia watumishi wake manabii.

24:3Ilikuwa baada ya mda mfupi kwenye kinywa cha Yahwe kwamba hili likaja juu ya Yuda, kuwaondoa usoni mwa uso wake, kwa sabau ya dhambi za Manase, yote aliyoyafanya,

24:4na pia kwa sababu ya damu isiyokuwa na hatia aliyoimwaga, kwa kuijaza Yerusalemu kwa damu isiyokuwa na hatia. Yahwe hakuwa tayari kusamehe hilo.

24:5Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Yehoyakimu, na yote aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?

24:6Yehoyakimu akalala pamoja na wazee wake, na Yekonia mtoto wake akawa mfalme katika sehemu yake.

24:7Mfalme wa Misri hakushambulia tena nje ya nchi yake, kwa sababu mfalme wa Babeli alakuwa amezishinda nchi zote ambazo zilikuwa zikitawaliwa na mfalme wa Misri, kutoka kwenye kitabu cha Misri mpaka Mto wa Frati.

2 Mambo ya Nyakati

2 Nya 36:5–8

5Yehoakimu alikuwa na umri wa miaka ishini na tano alipoanza kutawala, na akatawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Akafanya ambayao yalikuwa uovu katika macho ya Yahwe Mungu wake.

6Kisha Nebukadreza, mfalme wa Babeli, akamvamia na kumfunga katika minyororo kumuongoza kwenda mbali Babeli.

7Nebukadreza pia akabeba baadhi ya vitu katika nyumba ya Yahwe kwenda Babeli, na akaviweka katika ikulu yake huko Babeli.

8Kwa mambo mengine kuhusu Yehoyakimu, mambo mabaya aliyofanya, na yaliyopatikana zidi yake, tazama, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli. Basi Yehoyakimu, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY