Bible Explorer

Gundua › Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando › Anguko la Yerusalemu

Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando · Anguko la Yerusalemu

Yehoahazi mfalme wa Yuda

2 Fal 23:31–35 · 2 Nya 36:1–4

2 Wafalme

2 Fal 23:31–35

31Yehoahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na tatu alipoanza kutawala, na alitawala miezi mitatu katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa akiitwa Hamutali; alikuwa binti wa Yeremia wa Libana.

32Yehoahazi alifanya yaliyo maovu usoni kwa Yahwe, kama kila kitu ambacho babu zake walichokifanya.

33Farao Neko akamfunga gerezani huko Ribla katika nchi ya Hamathi, hivyo asiweze kutawala katika Yerusalemu. Kisha Neko akaitoza Yuda talanta mia moja za fedha na talanta moja ya dhahabu.

34Farao Neko akamfanya Eliakimu mwana wa Yosia mfalme katika mahali pa Yosia baba yake, na kubadilisha jina lake kuwa Yehoyakimu. Lakini akamchukua mfalme Yehoahazi kwenda Misri, na Yehoahazi akafia huko.

35Yehoyakimu akalipa fedha na dhahabu kwa Farao. Ili akutane na amri ya Farao, Yehoyakimu akaitoza nchi na kulazimisha kila mtu miongoni mwa watu wa nchi wamlipe fedha na dhahabu kulingana na makadirio yao.

2 Mambo ya Nyakati

2 Nya 36:1–4

1Kisha watu wa nchi wakamchukua Yehoazi mwana wa Yosia, na wakamfanya mfalme katika nafasi ya baba yake katika Yerusalemu.

2Yehoazi alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala, na akatawala miezi mitatu katita Yerusalemu.

3Mfalme wa Misiri akamwondoa katika Yerusalemu, na akaitoza nchi faini ya talanta za fedha mia moja na talanta moja ya dhahabu.

4Mfalme wa Misiri akamfanya Eliakimu, ndugu yake, mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu, na akambadili jina lake kuwa Yehoakimu. Kisha akamchukua ndugu yake Eliakimu - Yeahazi na kumpeleka Misiri.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY