Bible Explorer

Gundua › Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando › Sauli na Daudi

Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando · Sauli na Daudi

Sanduku laletwa Yerusalemu

2 Sam 6:12–19 · 1 Nya 15:25–29; 16:1–3

2 Samweli

2 Sam 6:12–19

12Kisha mfalme Daudi akaambiwa, “Yahwe ameibariki nyumba ya Obedi Edomu na kila kitu alichonacho kwa sababu ya sanduku la Mungu.” Hivyo Daudi akaenda na kulipandisha sanduku la Mungu kutoka katika nyumba ya Obedi Edomu hadi mji wa Daudi kwa furaha.

13Ikawa waliolibeba sanduku la Yahwe walipochukua hatua sita, akatoa sadaka ng'ombe na ndama aliyenona.

14Daudi akacheza mbele ya Yahwe kwa nguvu zake zote; alikuwa amevaa naivera ya kitani pekee.

15Hivyo Daudi na nyumba yote ya Israeli wakalipandisha sanduku la Yahwe kwa vifijo na sauti za tarumbeta.

16Hata ikawa sanduku la Yahwe lilipofika mjini mwa Daudi, Mikali, binti Sauli, alichungulia dirishani. Akamwona mfalme Daudi akiruka na kucheza mbele ya Yahwe. Akamdharau moyoni mwake.

17Wakaliingiza sanduku la Yahwe na kuliweka mahali pake, katikati ya hema ambayo Daudi alikuwa ameliwekea. Kisha Daudi akatoa sadaka ya kuteketezwa na matoleo ya amani mbele za Yahwe.

18Ikawa Daudi alipomaliza kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, akawabariki watu kwa jina la Yahwe wa majeshi.

19Kisha akawagawia watu wote, umati wote wa Israeli, wanaume kwa wanawake, kipande cha mkate, nyama na keki ya zabibu. Kisha watu wote wakaondoka; kila mmoja akarudi kwake.

1 Mambo ya Nyakati

1 Nya 15:25–29; 16:1–3

15:25Hivyo Daudi, wazee wa Israeli, na wakuu wa maelfu wakaenda kuchukua sanduku la agano la Yahweh kutoka nyumba ya Obedi Edomu kwa shangwe.

15:26Wakati Mungu alipo wasaidia Walawi kubeba sanduku la agano la Yahweh, walitoa ng'ombe saba na mbuzi

15:27Daudi alivishwa joho safi la maridadi, pamoja na Walawi walio beba sanduku, waimbaji, na Kenania, kiongozi wa nyimbo na waimbaji. Daudi alivaa juu ya joho lake naivera.

15:28Hivyo Israeli yote wakaleta sanduku la agano la Yahweh na kelele za shangwe, na sauti za tarumbeta, ngoma za saani, na vyombo vya uzi na vinubi.

15:29Lakini sanduku la Yahweh lilivyokuja kwa mji wa Daudi, Mikali binti wa Sauli, alitazama nje ya dirisha, Akamuona Mfalme Daudi akicheza na kusherehekea. Kisha akamdharau moyoni mwake.

16:1Wakaleta ndani Sanduku la Mungu na kuweka katika ya hema ambalo Daudi aliandaa. Kisha wakatoa sadaka ya kuteketeza na sadaka ya ushirika mbele ya Mungu.

16:2Daudi alipo maliza kutoa dhabiu ya kuteketeza na sadaka za ushirika, aliwabariki watu kwa jina la Yahweh.

16:3Alisambaza kwa kila Misraeli, mwanaume na mwanamke, kipande cha mkate, na kipande cha nyama, na keki ya mzabibu.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY