Gundua › Injili kando kwa kando › Njiani kwenda Yerusalemu
Injili kando kwa kando · Njiani kwenda Yerusalemu
Yesu atabiri kifo chake mara ya tatu
Mt 20:17–19 · Mk 10:32–34 · Lk 18:31–34
Mt 20:17–1917Yesu alipokuwa akipanda kwenda Yerusalem, aliwachukuwa wanafunzi wake kumi na mbili pembeni, na njiani akawaambia,
18''Tazama tunaelekea Yerusalemu, na Mwana wa Adamu atatiwa katika mikono ya wakuu wa makuhani na waandishi. Watamhukumu kifo
19na watamtoa kwa watu wa mataifa ili kumdhihaki, kumchapa na kumsulibisha. Lakini katika siku ya tatu atafufuka.''
Mk 10:32–3432Walipokuwa njiani, kwenda Yerusalemu, Yesu alikuwa amewatangulia mbele yao. Wanafunzi walishangaa, na wale waliokuwa wanafuata nyuma waliogopa. Ndipo Yesu akawatoa pembeni tena wale kumi na wawili na akaanza kuwaambia ambacho kitamtokea hivi karibuni:
33“Tazama, tunakwenda mpaka Yerusalemu, na Mwana wa Adamu atafikishwa kwa makuhani wakuu na waandishi. Watamhukumu afe na watamtoa kwa watu wa Mataifa.
34Watamdhihaki, watamtemea mate, watampiga fimbo, na watamwua. Lakini baada ya siku tatu atafufuka.”
Lk 18:31–3431Baada ya kuwakusanya wale kumi na wawibili, akawaambia, 'Tazama, tunapanda kwenda Yerusalemu, na mambo yote ambayo yameandikwa na manabii kuhusu Mwana wa Adamu yatakamilishwa.
32Kwa maana atatiwa mikononi mwa watu wa Mataifa na atatendewa dhihaka na jeuri, na kutemewa mate.
33Baada ya kumchapa viboko watamwua na siku ya tatu atafufuka. '
34Hawakuelewa mambo haya, na neno hili lilikuwa limefichwa kwao, na hawakuelewa mambo yaliyosemwa.
Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.
Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY