Bible Explorer

Gundua › Njia za safari › Kutoka

Njia za safari

Kutoka

Kutoka Misri kupitia jangwa hadi Moabu · Vituo: 14 · ≈ 830 km kwa mistari iliyonyooka

1234567891011121314

Njia ya Kutoka inabishaniwa: vituo vyake vingi havijapatikana. Ramani inaonyesha mahali ambapo OpenBible.info inaona kuwa panawezekana zaidi; wataalamu wanapendekeza mengine, pamoja na kuvuka kaskazini zaidi na mlima Sinai mwingine.

Mistari inaunganisha vituo kwa mpangilio wa maandiko — njia zenyewe hazijulikani. Vistari: kwa meli. Hafifu: mahali hapajulikani kwa hakika.

Vituo

  1. RamesiKut 12:37Waisraeli wakasafiri kutoka Ramesi kwenda Sakothi. Walikuwa na idadi ya wanaume 600,000 kwa miguu, kuongezea kwa wanawake na watoto.
  2. SakothiKut 12:37Waisraeli wakasafiri kutoka Ramesi kwenda Sakothi. Walikuwa na idadi ya wanaume 600,000 kwa miguu, kuongezea kwa wanawake na watoto.
  3. EthamuKut 13:20Waisraeli walisafiri kutoka Sakothi na kuweka kambi Ethamu pembezoni mwa nyikani.
  4. Pi HahirothiKut 14:2“Waambie Waisraeli wageuke na kueka kambi mbele ya Pi Hahirothi, katikati ya Migdoli na bahari, mbele ya Baali Zefoni. Wapaswa kueka kambi pembenni ya Pi Hahirothi.
  5. MaraKut 15:23Kisha wakaja Mara, lakini hawakunywa maji ya huko kwasababu yalikuwa machungu. Hivyo wakaita hiyo sehemu Mara.
  6. ElimuKut 15:27Kisha watu wakaja Elimu, palipo kuwa na chemichemi kumi na mbili za maji na miti sabini ya mtende. Walieka kambi hapo pembeni ya maji.
  7. SiniKut 16:1Watu wakaendelea na safari kutoka Elimu, na jamii yote ya Waisraeli ikaja nyikani mwa Sinu, iliyopo katikati ya Elimu na Sinai, siku ya kumi na tano ya mwezi wa pili walipo toka Misri.
  8. RefidimuKut 17:1Jamii yote ya Israeli ili safiri kutoka nyikani ya Sinu, wakifuata maelekezo ya Yahweh. Walieka kambi Refidimu, lakini hapakuwa na maji ya watu kunywa.
  9. SinaiKut 19:1Katika mwezi wa tatu baada ya watu wa Israeli kutoka Misri, siku hiyo, walikwenda nyikani ya Sinai.
  10. ParaniHesabu 10:12Wana wa Israeli wakaendelea na safari yao toka jangwa la Sinai. Lile wingu likasimama kwenye jangwa la Parani.
  11. KadeshiHesabu 20:1Kwa hiyo wana wa Israeli, na jamii yote ya watu, wakaenda katika jangwa la Sini katika mwezi wa kwanza; wakaa Kadeshi. Hapo ndipo Miriamu alipofia na kuzikwa.
  12. Mlima HoriHesabu 20:22Kwa hiyo watu wakasafiri kutoka Kadeshi. Wana wa Israeli, watu wote, wakafika Mlima Hori.
  13. MoabuHesabu 22:1Watu wa Israeli wakasafiri mpaka wakaweka kambi kwenye uwanda wa Moabu karibu na Yeriko, kwenye upande mwingine wa mto Yorodani kutoka mji ule.
  14. Mlima NeboKum 32:49“Nenda katika usawa huu wa milima wa Abarimu, juu ya mlima wa Nebo, ambao upo katika nchi ya Moabu, mkabala na Yeriko. Utatazama nchi ya Kanani, ambayo ninawapatia watu wa Israeli kama miliki yao.

Kila nukta ni mahali panapowezekana zaidi (OpenBible.info); nukta hafifu inamaanisha utambulisho hauna uhakika. Mahali pasipojulikana hapapo kwenye ramani.

Mahali: OpenBible.info Bible Geocoding Data (CC BY 4.0).

Mipaka ya nchi kavu: Natural Earth (mali ya umma).