Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2027 › 3 Desemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 3 Desemba 2027
Ijumaa · Juma la 1 la Majilio
Sikukuu na watakatifu
Ijumaa ya Juma la 1 la Majilio
Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe
Mt. Fransisko Ksaveri, padre · Kumbukumbu
Kufunga na toba
Siku ya toba
Kila Ijumaa ni siku ya toba; kila baraza la maaskofu huamua jinsi inavyoadhimishwa: kujinyima nyama au tendo lingine la toba. Kufunga kunawahusu wenye miaka 18 hadi 59, kujinyima nyama kuanzia miaka 14.
Masomo ya siku
Somo la kwanza
17Katika mda mdogo uliobakia, Lebanoni itajeuzwa kuwa shamba, na shamba litakuwa msitu. 18Siku hiyo viziwi watasikia maneno ya kitabu, na macho ya vipofu yataona katika giza nene. 19Waliodhulumiwa watafuurahia pamoja na Yahwe, na masikini miongoni mwa watu watafurahia kwa Mtakatifu wa Israeli. 20Maana watu wasio katili watakwisha, na wenye dharau watatoweka. Wale wote wanopendakuteda maovu wataondolewa, 21nani na kwa neno linamfanya mtu kuwa mkosaji. Watamuekea mtego kwa yeye anayeitafuta haki katika geti na kuweka haki chini kwa uongo usio na kitu. 22Hivyo basi Yahwe asema hivi kuhusu nyumba ya Yakobo- Yahwe aliyemkomboa Ibrahimu, ''Yakobo hataaibika tena, wala uso wake hautabadilika rangi yake. 23Lakini anapowaona watoto wake, kazi ya mikono yangu, watalitakasa jina langu, Watalitakasa jina langu Mtakatifu wa Yakobo, na wtasimama katika hofu ya Mungu wa Israeli. 24Wale watakaopotea kiroho watapata uelewa na walalamikaji watajifunza maarifa.''
Wimbo wa katikati
1Zaburi ya Daudi. Yahwe ni nuru yangu na wokovu wangu; nimuogope nani? Yahwe ni salama ya maisha yangu; ni mhofu nani? 4Kitu kimoja nimekiomba kwa Yahwe, nami nitakitafuta hicho: kwamba niweze kukaa katika nyumba ya Yahwe siku zote za maisha yangu, kuutazama uzuri wa Yahwe na kutafakari hekaruni mwake. 13Kitu gani kingeweza kunitokea kama nisingeamini kuwa nitauona uzuri wa Yahwe katika nchi ya walio hai? 14Umngoje Yahwe; uwe imara, na moyo wako uwe jasiri! Umngoje Yahwe!
Injili
27Ndipo Yesu alipokuwa akipita kutoka pale, wanaume wawili vipofu wakamfuata. Waliendelea kupaza sauti wakisema, “Tunaomba uturehemu, Mwana wa Daudi.” 28Pindi Yesu apokuwa amefika kwenye nyumba, wale vipofu wakaja kwake. Yesu akawaambia, “Mnaamini kwamba ninaweza kutenda?” Nao wakamwambia “Ndiyo, Bwana” 29Ndipo Yesu akagusa macho yao na kusema “Na ifanyike hivyo kwenu kama imani yenu ilivyo” 30Na macho yao yakafumbuka. Ndipo Yesu akasisitiza akawaamuru na kusema “Angalieni mtu yeyote asifahamu kuhusu jambo hili.” 31Lakini watu hawa wawili wakaondoka na kutangaza habari hizi sehemu zote za mji.
Watakatifu wa siku
- Mt. Fransisko Ksaveri, padre
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili C, mwaka wa siku za kazi II.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki