Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2027 › 30 Novemba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 30 Novemba 2027

Jumanne · Juma la 1 la Majilio

Sikukuu na watakatifu

Mt. Andrea, mtume

Sikukuu · Rangi ya liturujia: nyekundu

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Rum 10:9–18

9Kwa kuwa kama kwa kinywa chako unamkiri Yesu ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka. 10Kwa kuwa kwa moyo mtu huamini na kupata haki, na kwa kinywa hukiri na kupata wokovu. 11Kwa kuwa andiko lasema, “Kila amwaminiye hata aibika.” 12kwa kuwa hakuna tofauti kati ya Myahudi na Myunani. Kwa kuwa Bwana yule yule ni Bwana wa wote, na ni tajiri kwa wote wamwitao. 13Kwa kuwa kila mtu ambaye huliitia jina la Bwana ataokoka. 14Kwa jinsi gani wanaweza kumwita yeye ambaye hawajamwamini? Na jinsi gani wanaweza kuamini katika yeye ambaye hawajamsikia? Na watasikiaje pasipo muhubiri? 15Na jinsi gani wanaweza kuhubiri, isipokuwa wametumwa? - Kama ilivyoandikwa, “Jinsi gani ni mizuri miguu ya wale ambao wanatangaza habari za furaha za mambo mema!” 16Lakini wote hawakusikiliza injili. Kwa kuwa Isaya hunena, “Bwana, ni nani aliyesikia ujumbe wetu?” 17Hivyo imani huja kutokana na kusikia, na kusikia kwa neno la Kristo. 18Lakini nasema, “Je hawakusikia?” Ndiyo, kwa hakika sana. “Sauti yao imekwisha toka nje katika nchi yote, na maneno yao kwenda miisho ya dunia.”

Wimbo wa katikati

Zab 19:1–4

1Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi. Mbingu za tangaza utukufu wa Mungu, na mawingu hufanya kazi ya mikono yake ijulikane! 2Siku hadi siku hotuba hutokea; usiku hadi usiku hufunua maarifa. 3Hakuna hotuba wala misemo; sauti zao hazisikiki. 4Bali maneno yao husambaa nje duniani kote, na hotuba zao hata mwisho wa dunia. Yeye ametengeneza hema kwa ajili ya jua kati yao.

Injili

Mt 4:18–22

18Alipokuwa akitembea kandokando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aliyekuwa akiitwa Petro, na Andrea kaka yake, wakitega nyavu baharini, kwa kuwa walikuwa wavuvi wa samaki. 19Yesu akawaambia, “Njooni mnifuate, nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.” 20Mara moja waliziacha nyavu na walimfuata. 21Na Yesu alipokuwa akiendelea kutoka hapo aliwaona ndugu wawili wengine, Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana kaka yake. Walikuwa katika mtumbwi pamoja na Zebedayo baba yao wakishona nyavu zao. Akawaita, 22na mara moja wakaacha mtumbwi na baba yao nao wakamfuata.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 30 Novemba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili C, mwaka wa siku za kazi II.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki