Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2027 › 29 Novemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 29 Novemba 2027
Jumatatu · Juma la 1 la Majilio
Sikukuu na watakatifu
Jumatatu ya Juma la 1 la Majilio
Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: zambarau
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1Vitu ambavyo Isaya mtoto Amozi alivijua katika maono, kuhusu Yuda na Yerusalemu. 2Na itakuwa katika siku za mwisho, ule mlima wa nyumba ya Yahwe itaanzishwa kama mlima mrefu zaidi, na utanyanyuliwa juu ya vilima, na mataifa yote yatakusanyika pale. 3Watu wengi watakuja na kusema, ''Njooni, twendeni juu ya mlima wa Yahwe, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo, kwa hiyo anaweza kutufundisha baadhi ya njia zake na tunaweza kutembea katika njia zake.'' Nje ya Sayuni itaenda sheria na neno la Yahwe litatoka Yerualemu. 4Atahukumu kati ya mataifa na atatoa maamuzi kwa watu wote; watayapiga nyungo mapanga yao kuwa majembe, na mikiku yao kama ya kukatia ndoano; taifa halitanyanyua upanga juu ya taifa lingine, na wala hawata jiandaa kwa vita tena. 5Nyumba ya Yakobo, njooni, na tutembee katika mwanga wa Yahwe.
Wimbo wa katikati
1Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu, wa Daudi. Nilifurahi waliponiambia, “Na twende kwenye Nyumba ya Yahwe.” 2Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama ndani ya malango yako! 4Makabila huenda juu Yerusalemu, makabila ya Yahwe; kama ushuhuda wa Israeli, kulishukuru jina la Yahwe. 5Huko viliwekwa viti vya hukumu, viti vya enzi vya nyumba ya Daudi. 6Ombeni kwa ajili ya amani ya Yerusalemu! “Wote wakupendao wawe na amani. 7Amani iwepo ndani ya kuta zako ili ikutetee, na wawe na amani ndani ya ngome zako.” 8Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu nitasema, “Amani iwe ndani yenu.” 9Kwa ajili ya Yahwe Mungu wetu, nitatafuta mema kwa ajili yako.
Injili
5Wakati Yesu alipofika Kapernaumu, Jemedari akaja kwake akamuuliza 6akisema, “Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani amepooza na ana maumivu ya kutisha.” 7Yesu akamwambia, “Nitakuja na kumponya”. 8Jemedari akajibu na kumwambia, “Bwana, mimi si wathamani hata uje na kuingia ndani ya dari yangu, sema neno tu na mtumishi wangu ataponywa. 9Kwa kuwa mimi pia ni mtu niliye na mamlaka, na ninao askari walio chini yangu. Nikisema kwa huyu “Nenda' na huenda, na kwa mwingine 'Njoo' na yeye huja, na kwa mtumishi wangu, 'Fanya hivi,' na yeye anafanya hivyo” 10Wakati Yesu aliposikia haya, alishangazwa na kuwaambia wale waliokuwa wakimfuata, “Kweli ninawaambia, Sijapata kuona mtu mwenye imani kama huyu katika Israel. 11Ninawambieni, wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, wataketi katika meza pamoja na Abrahimu, Isaka, na Yakobo, katika ufame wa mbinguni.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili C, mwaka wa siku za kazi II.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki