Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2027 › 20 Novemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 20 Novemba 2027
Jumamosi · Juma la 33 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumamosi ya Juma la 33 la Mwaka
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani
Kumbukumbu ya Bikira Maria siku ya Jumamosi · Kumbukumbu ya hiari
Masomo ya siku
Somo la kwanza
Haimo katika tafsiri hii
Wimbo wa katikati
1Kwa kiongozi wa muziki; weka kwenye mtindo wa Muth Labben. Zaburi ya Daudi. Nitamshukuru Yahweh kwa moyo wangu wote; nitayasimulia matendo yako makuu. 2Nitafurahi na kushangilia katika wewe; nitaliimbia jina lako, Wewe uliye juu. 3Maadui zangu wanaponirudia, hujikwaa na kuangamia mbele zako. 5Uliwakemea mataifa; umewaharibu waovu; na kuwa futilia mbali jina lao milele na milele. 15Mataifa yamedidimia chini katika shimo ambalo walilolitengeneza; miguu yao imenaswa kwenye nyavu walioificha wenyewe. 18Kwa kuwa mhitaji hata sahauliwa siku zote, wala matumaini ya wanyonge hayatapotea milele.
Injili
27Baadhi ya Masadukayo wakamwendea, wale ambao wanasema kwamba hakuna ufufuo, 28wakamwuliza, wakisema, “Mwalimu, Musa alituandikia kwamba kama mtu akifiwa na ndugu mwenye mke ambaye hana mtoto basi anapaswa kumchukuna mke wa ndugu yake na kuzaa nae kwa ajili ya kaka yake. 29Kulikuwa na ndugu saba Wa kwanza alioa, akafa bila kuacha mtoto, 30na wa pili pia. 31Wa tatu akamchukua vilevile, vivyo hivyo wa saba hakuacha watoto na akafa. 32Baadaye yule mwanamke pia akafa. 33Katika ufufuo atakuwa mke wa nani? Maana wote saba walikuwa wamemwoa. ' 34Yesu akawaambia, “Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa. 35Lakini wale wanastaohili kupokea ufufuo wa wafu na kuingia uzima wa milele hawaoi wala hawaolewi. 36Wala hawawezi kufa tena, kwa sababu huwa sawasawa na malaika na ni watoto wa Mungu, wana wa ufufuo. 37Lakini hiyo wafu wanafufuliwa, hata Musa alionyesha mahali katika habari za kichaka, pale alimwita Bwana kama Mungu wa Ibrahimu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo. 38Sasa, yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai, kwa sababu wote huishi kwake. “ 39Baadhi ya walimu wa Sheria wakamjibu, 'Mwalimu, umejibu vema. ' 40Hawakuthubutu kumwuliza maswali mengine zaidi.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki