Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2027 › 19 Novemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 6 Novemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 19 Novemba 2027
Ijumaa · Wiki ya 22 baada ya Pentekoste · Sauti ya 4
Sikukuu na watakatifu
Askofu Mtakatifu Paulo Mwungamaji, Patriarki wa Konstantinopoli (350)
Siku ya mfungo
Mfungo: pamoja na mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
10Aristarko, mfungwa mwenzangu, anawasalimu, pia na Marko binamu yake na Barnaba mliyepokea utaratibu kutoka kwake, “kama akija kwenu, mpokeeni,” 11Na pia Yesu aitwaye Yusto. Hawa peke yao wa tohara ni watendakazi wenzangu kwa jili ya ufalme wa Mungu. Wamekuwa ni faraja kwangu. 12Epafra anawasalimu. Yeye ni mmoja wenu na mtumwa wa Kristo Yesu. Yeye hufanya bidii katika maombi kwa ajili, ili kwamba mweze kusimama kwa ukamilifu na kuhakishwa kikamilifu katika mapenzi yote ya Mungu. 13Kwa kuwa ninamshuhudia, kwamba anafanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu, kwa hao walioko Laodekia, na kwa hao walioko Hierapoli. 14Luka yule tabibu mpendwa, na Dema wanawasalimu. 15Wasalimu ndugu zangu walioko Laodekia, na Nimfa, na kanisa lile lililoko nyumbani kwake. 16Barua hii itakapokuwa imesomwa miongoni mwenu, isomwe pia kwa kanisa la walaodekia, nanyi pia hakikisheni mnaisoma ile barua kutoka Laodekia. 17Sema kwa Arkipo, ''Angalia ile huduma ambayo umeipokea katika Bwana, kwamba unapaswa kuitimiza.” 18Salamu hii ni kwa mkono wangu mwenyewe - Paulo. Ikuumbukeni minyororo yangu. Neema na iwe nanyi.
Injili
2Na hapatakuwepo na siri iliyofichika ambayo haitafunuliwa, wala jambo lililofichwa ambalo halitajulikana. 3Na lolote mlilolisema katika giza, litasikiwa katika mwanga. Na yoyote mliyoyasema kwenye sikio ndani ya vyumba vyenu vya ndani vilivyofungwa yatatangazwa juu ya paa la nyumba. 4Nawaambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili na kisha hawana kitu kingine cha kufanya, 5Lakini nitawaonya mtakaye mwogopa. Mwogopeni yule ambaye baada ya kuwa ameua, ana mamlaka ya kutupa jehanamu. Ndiyo, nawaambiani ninyi, mwogopeni huyo. 6Je shomoro watano hawauzwi kwa sarafu mbili? hata hivyo hakuna hata mmoja wao atakayesahaulika mbele za Mungu. 7Lakini mjue kuwa, nywele za vichwa vyenu vimehesabiwa. Msiogope. Ninyi ni wa thamani kubwa kuliko shomoro wengi. 8Ninawaambia, yeyote atakayenikiri Mimi mbele za watu, Mwana wa Adamu atamkiri mbele za malaika wa Mungu. 9Lakini yeyeyote atakayenikana mbele za watu naye atakanwa mbele ya Malaika wa Mungu. 10Yeyote atakayesema neno baya juu ya Mwana wa Adamu, atasamehewa, lakini yeyote atakayemkufuru Roho Mtakatifu, hatasamehewa. 11Watakapowapeleka mbele za wakuu wa masinagogi, watawala, na wanye mamlaka, msiogope juu na namna ya kuongea katika kujitetea au nini mtakachosema, 12kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha namna mtakavyosema kwa wakati huo.”
Watakatifu wa siku
- Mtakatifu Mtawa Barlaamu wa Khutyn (1192)
- Wafiadini wa Kikasisi Niketa, Askofu wa Orekhovo-Zuyevo, Anatoli, Arsenio, Nikolao, Nikolao, Konstantino, mapadri, Watawa Wafiadini Barlaamu, Gabrieli na Gabrieli, Watawa Wafiadini Nina na Serafima (1937)
- Mtakatifu Mtawa Luka wa Tauromenio (800-820)
- Mfiadini wa Kikasisi Basili, padri (1938)
- Wafiadini Tekusa, Aleksandra, Polaktia, Klaudia, Eufrosini, Athanasia na Matrona (karne ya 3)
- Kumbukumbu ya kupatikana kwa Msalaba wenye Thamani na misumari na Malkia Mtakatifu Helena Sawa na Mitume huko Yerusalemu (326)
- Mtakatifu Mtawa Luka, mtunza mali wa Mapango ya Kyiv (karne ya 13)
- Askofu Mtakatifu Germano, Askofu Mkuu wa Kazan (1567)
- Mtakatifu Mtawa Barlaamu wa Keret (karne ya 16)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 6 Novemba katika kalenda ya kanisa ni 19 Novemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki