Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2027 › 20 Oktoba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 7 Oktoba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 20 Oktoba 2027
Jumatano · Wiki ya 18 baada ya Pentekoste · Sauti ya 8
Sikukuu na watakatifu
Wafiadini Sergio na Bakko (290-303)
Siku ya mfungo
Mfungo: pamoja na mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
25Waume, wapendeni wake zenu kama vile Kristo alivyolipenda kanisa na akajitoa mwenyewe kwa ajili yake. 26Alifanya hivyo ili liwe takatifu. Alilitakasa kwa kuliosha na maji katika neno. 27Alifanya hivi ili kwamba aweze kujiwasilishia mwenyewe kanisa tukufu, pasipo na doa wala waa au kitu kifananacho na haya, badala yake ni takatifu lisilo na kosa. 28Kwa njia ile ile, waume wanatakiwa kuwapenda wake zao kama miili yao. Yule ampendae mke wake anajipenda mwenyewe. 29Hakuna hata mmoja anayechukia mwili wake. Badala yake, huurutubisha na kuupenda, kama Kristo pia alivyolipenda kanisa. 30Kwa kuwa sisi ni washiriki wa mwili wake. 31“Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na ataungana na mke wake, na hao wawili watakuwa mwili mmoja”. 32huu ulikuwa umefichika. Lakini ninasema kuhusu Kristo na kanisa. 33Walakini, kila mmoja wenu lazima ampende mke wake kama mwenyewe, na mke lazima amheshimu mumewe.
Injili
46Kwanini mnaniita, 'Bwana, Bwana', na bado hamyatendi yale nisemayo? 47Kila mtu ajaye kwangu na kuyasikia maneno yangu na kuyatendea kazi, nitawaonyesha jinsi alivyo. 48Anafanana na mtu ajengae nyumba yake, ambaye huchimba chini sana, na kujenga msingi wa nyumba juu ya mwamba imara. Mafuriko yalipokuja, maporomoko ya maji yaliipiga nyumba, lakini hayakuweza kuitikisa, kwa sababu ilikuwa imejengwa vizuri. 49Lakini yeyote asikiaye neno langu na hakulitii; mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ulipoishukia kwa nguvu, nyumba ile ilitopata maangamizi makubwa. 7:1Baada ya Yesu kumaliza kila kitu alichokuwa anasema kwa watu waliomsikiliza, akaingia Kapernaumu.
Watakatifu wa siku
- Mfiadini wa Kikasisi Nikolao, padri (1942)
- Wafiadini Yuliani, padri, na Kaisario, shemasi (karne ya 1)
- Mfiadini Pelagia, bikira wa Tarso (karibu 290)
- Mfiadini Polikronio, padri (karne ya 4)
- Mtakatifu Mtawa Sergio, mtiifu, wa Mapango ya Kyiv (karibu karne ya 13)
- Mtakatifu Mtawa Sergio wa Nurma (wa Vologda) (1412)
- Kupatikana kwa masalia ya Mtakatifu Mtawa Martiniani wa Belozersk (1514)
- Askofu Mtakatifu Yona, mtenda miujiza wa Hankou (ROCOR)
- Ikoni ya Mama wa Mungu ya Mapango ya Pskov iitwayo “Huruma” (1524, 1812)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 7 Oktoba katika kalenda ya kanisa ni 20 Oktoba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki