Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2027 › 21 Oktoba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 8 Oktoba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 21 Oktoba 2027
Alhamisi · Wiki ya 18 baada ya Pentekoste · Sauti ya 8
Sikukuu na watakatifu
Mtakatifu Mtawa Pelagia (457)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Injili
17Hizi habari njema za Yesu zilienea Yudea yote na kwa mikoa yote ya jirani. 18Wanafunzi wa Yohana walimwamwambia mambo haya yote. 19Ndipo Yohana akawaita wawili wa wanafunzi wake na kuwatuma kwa Bwana kusema “Wewe ndiye yule ajaye, au kuna mtu mwingine tumtazamie? 20Walipofika karibu na Yesu hawa wakasema, “Yohana mbatizaji ametutuma kwako kusema, 'Wewe ni yule ajaye au kuna mtu mwingine tumtazamie?” 21kwa wakati huo aliowaponya watu wengi kutoka katika magonjwa na mateso, kutoka kwa roho wachafu, na kwa watu wenye upofu aliwapa kuona. 22Yesu akajibu na kusema kwao. “Baada ya kuwa mmekwenda mlikotoka mtamjulisha Yohana mlichokiona na kukisikia. Wenye upofu wanapokea kuona na viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na kuwa hai tena, masikini wanaambiwa habari njema. 23Na mtu ambaye hataacha kuniamini mimi kwa sababu ya matendo yangu amebarikiwa”. 24Baada ya wale waliotumwa na Yohana kurudi walikotoka, Yesu akaanza kusema kwa makutano juu ya Yohana, “Mlikwenda nje kuona nini, mwanzi ukiwa unatikiswa na upepo? 25lakini mlikwenda nje kuona nini, mtu aliyevaa vizuri? tazama watu wale wanaovaa mavazi ya kifalme na kuishi maisha ya starehe wako kwenye nafasi za wafalme. 26lakini mnakwenda nje kuona nini, Nabii? Ndiyo, ninasema kwenu na zaidi sana kuliko nabii. 27Huyu ndiye aliyeandikiwa, “Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya macho yenu, atakeyeandaa njia kwa ajili yangu, 28Nasema kwenu, kati ya wale waliozaliwa na mwanamke, hakuna mkuu kama Yohana, lakini mtu asiye muhimu sana atakayeishi na Mungu mahali alipo yeye, atakuwa mkuu kuliko Yohana.” 29Na watu wote waliposikia haya pamoja na watoza ushuru, walitangaza kuwa Mungu ni mwenye Haki. Walikuwepo kati yao wale waliobatizwa kwa ubatizo wa Yohana. 30Lakini mafarisayo na wataalamu wa sheria za kiyahudi, ambao hawakubatizwa na yeye walikataa hekima za Mungu kwa ajili yao wenyewe.
Waraka
33Walakini, kila mmoja wenu lazima ampende mke wake kama mwenyewe, na mke lazima amheshimu mumewe. 6:1Watoto watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa maana hii ni haki. 2“Mheshimu baba yako na mama yako” (Maana hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi), 3“ili iwe heri kwenu na muweze kuishi maisha marefu juu ya nchi.” 4Na ninyi akina baba, msiwakwaze watoto na kuwasababishia hasira, badala yake, waleeni katika maonyo na maagizo ya Bwana. 5Enyi watumwa, iweni watiifu kwa mabwana zenu wa hapa duniani kwa heshima kubwa na kutetemeka kwa hofu itokayo mioyoni mwenu. muwe watiifu kwao kama vile mnavyomtii Kristo. 6Utii wenu usiwe tu pale mabwana zenu wanapowatazama ili kuwafurahisha. Badala yake, iweni watiifu kama watumwa wa Kristo. Fanyeni Mapenzi ya Mungu kutoka mioyoni mwenu, 7watumikieni kwa mioyo yenu yote, kwa kuwa mnamtumikia Bwana na wala si wanadamu, 8mnapaswa kujua kwamba katika kila tendo jema mtu analofanya, atapokea zawadi kutoka kwa Bwana, ikiwa ni mtumwa au mtu huru. 9Na ninyi mabwana fanyeni vivyo hivyo kwa watumwa wenu. Msiwatishe mkijua kwamba yeye aliye Bwana wa wote ni yule aliye mbinguni. Mkijua kuwa hakuna upendeleo ndani yake.
Watakatifu wa siku
- Wafiadini wa Kikasisi Demetrio, Askofu Mkuu wa Mozhaysk, na pamoja naye Yohana, shemasi, Watawa Wafiadini Ambrosio na Pakomio, Mtawa Mfiadini Tatiana, Mfiadini Nikolao, Wafiadini Maria na Nadezhda (1937)
- Wafiadini wa Kikasisi Yona, Askofu wa Velizh, Petro, Basili, Paulo, Petro, Vladimir, mapadri, Mtawa Mfiadini Serafim, Wafiadini Vikta, Yohana, Nikolao na Mfiadini Elisabeti (1937)
- Mtawa Mfiadini Barlaamu (mwishoni mwa miaka ya 1930)
- Mtakatifu Pelagia, bikira (303)
- Mtakatifu Mtawa Taisia (karne ya 4)
- Mtakatifu Mtawa Dositheo wa Verkhneostrovsk, wa Pskov (1482)
- Mtakatifu Mtawa Trifoni, arkimandriti wa Vyatka, mtenda miujiza (1612)
- Mkutano wa Watakatifu wa Vyatka
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 8 Oktoba katika kalenda ya kanisa ni 21 Oktoba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki