Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2027 › 14 Oktoba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 14 Oktoba 2027

Alhamisi · Juma la 28 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Alhamisi ya Juma la 28 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Mt. Kalisto I, papa na shahidi · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Rum 3:21–30

21Lakini sasa pasipo sheria, haki ya Mungu imejulikana. Ilishuhudiwa kwa sheria na Manabii, 22hiyo ni, haki ya Mungu kupitia imani katika Yesu Kristo kwa wale wote wanaoamini. Maana hakuna tofauti. 23Kwa kuwa wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. 24Wamehesabiwa haki bure kwa neema yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu. 25Kwa maana Mungu alimtoa Kristo Yesu awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake. Alimtoa Kristo kama ushahidi wa haki yake, kwa sababu ya kuziachilia dhambi zilizopita 26katika uvumilivu wake. Haya yote yalitokea ili kuonesha haki yake wakati huu wa sasa. Hii ilikuwa ili aweze kujithibitisha mwenyewe kuwa haki, na kuonesha kwamba humhesabia haki mtu yeyote kwa sababu ya imani katika Yesu. 27Kuwapi basi kujisifu? Kumetengwa. Kwa misingi ipi? Misingi ya matendo? Hapana, lakini kwa misingi ya imani. 28Hivyo tunahitimisha kwamba mtu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria. 29Au Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Je yeye si Mungu wa watu wa Mataifa pia? Ndiyo, wa mataifa pia. 30Ikiwa kwa kweli Mungu ni mmoja, atawahesabia haki walio wa tohara kwa imani, na wasiotahiriwa kwa njia ya imani.

Wimbo wa katikati

Zab 130:1–6

1Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu. Toka ndani yangu ninakulilia, Yahwe. 2Bwana, usikie sauti yangu; masikio yako na yasikie kwa makini kuomba kwangu kwa ajili ya huruma. 3Kama wewe, Yahwe, ungehesabu maovu, Bwana, ni nani angesimama? 4Lakini kwako kuna msamaha, ili uweze kuheshimiwa. 5Ninamngoja Yahwe, nafsi yangu inasubiri, na katika neno lake ninatumainia. 6Nafsi yangu inamngoja Bwana kuliko mlinzi aingojavyo asubuhi.

Injili

Lk 11:47–54

47Ole wenu, kwa sababu mnajenga na kuweka kumbukumbu kwenye makaburi ya manabii' ambao waliuwawa na mababu zenu. 48Hivyo ninyi mwashuhudia na kukubaliana na kazi walizozifanya mababu zenu, kwa sababu hakika waliwauwa manabii ambao mnajenga kumbukumbu katika makaburi yao. 49Kwa sababu hiyo pia, hekima ya Mungu inasema, 'Nitawatumia manabii na mitume nao watawatesa na kuwaua baadhi yao. 50Kizazi hiki kitawajibika kwa damu ya manabii waliouawa tangu kuanza kwa dunia, 51Kutoka damu ya Abeli hadi damu ya Zakaria, aliyeuawa katikati ya madhabahu na patakatifu. Ndiyo, nawaambia ninyi, kizazi hiki kitawajibika. 52Ole wenu waalimu wa sheria za Kiyahudi, kwa sababu mmechukua funguo za ufahamu; nyie wenyewe hamuingii, na wale wanaotaka kuingia mnawazuia.” 53Baada ya Yesu kuondoka pale, Waandishi na Mafarisayo walimpinga na kubishana naye juu ya mambo mengi. 54wakijaribu kumnsana kwa maneno yake.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 14 Oktoba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki