Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 22 Septemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 9 Septemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 22 Septemba 2027
Jumatano · Wiki ya 14 baada ya Pentekoste · Sauti ya 4
Sikukuu na watakatifu
Baada ya Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Mama Mtakatifu Sana wa Mungu
Siku ya mfungo
Mfungo: pamoja na mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
3Nawaambia ninyi hili kwa sababu mnatafuta ushahidi kwamba Kristo ananena kupitia mimi. Yeye sio dhaifu kwenu, badala yake, yeye ni mwenye nguvu ndani yenu. 4Kwa kuwa alisulibiwa katika udhaifu, lakini yu hai kwa nguvu za Mungu. Kwa kuwa sisi pia tu dhaifu ndani yake, lakini tutaishi naye kwa nguvu za Mungu miongoni mwenu. 5Jichunguzeni wenyewe muone kama mko katika imani. Jipimeni wenyewe. Hamgundui kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Yeye yumo, vinginevyo kama hamjathibitishwa. 6Na nina ujasiri kwamba ninyi mtagundua kwamba sisi hatukukataliwa. 7Sasa tunaomba kwa Mungu kwamba msiweze kufanya chochote kibaya. Siombi kwamba sisi tuweze kuonekana tumepita jaribu, badala yake ninaomba kwamba muweze kufanya kilicho sahihi, Ingawa tunaweza kuonekana tumeshindwa jaribu. 8Kwa kuwa sisi hatuwezi kufanya lolote kinyume na kweli, lakini ni kwa ajili ya kweli tu. 9Kwa kuwa tunafurahi wakati tunapokuwa dhaifu nanyi mkiwa na nguvu. Tunaomba pia kwamba muweze kufanywa wakamilifu. 10Nayaandika mambo haya wakati nikiwa mbali nanyi, ili kwamba wakati nikiwa pamoja nanyi sihitaji kuwaonesha ukali ninyi. Sihitaji kutumia mamlaka Bwana aliyonipaa mimi niwajenge na siyo kuwaharibu chini. 11Hatimaye, ndugu wa kiume na wa kike, furahini! fanyeni kazi kwa ajili ya urejesho, mtiwe moyo, kubalianeni ninyi kwa ninyi, muishi katika amani. Na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi. 12Salimianeni kila mmoja kwa busu takatifu. 13Waumini wote wanawasalimu. 14Neema ya Bwana Yesu Kristo, upendo wa Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu uwe pamoja nanyi nyote.
Injili
35Katika siku hiyo, wakati wa jioni ulipowadia, akasema kwao, “Twendeni upande wa pili”. 36Hivyo wakauacha umati, wakamchukua Yesu, wakati huo tayari alikuwa ndani ya mtumbwi. Mitumbwi mingine ilikuwa pamoja naye. 37Na upepo mkali wa dhoruba na mawimbi yalikuwa yakiingia ndani ya mtumbwi na mtumbwi tayali ulikuwa umejaa. 38Lakini Yesu mwenyewe alikuwa kwenye shetri, amelala kwenye mto. Wakamwamsha, wakisema, “Mwalimu, haujali sisi tunakufa?” 39Na akaamka, akaukemea upepo na akaiambia bahari, “'Iwe shwari, amani”. Upepo ukakoma, na kulikuwa na utulivu mkubwa. 40Na akasema kwao, “Kwa nini mnaogopa? Je hamna imani bado?” 41Walijawa na hofu kubwa ndani yao na wakasemezana wao kwa wao, “ Huyu ni nani tena, kwa sababu hata upepo na bahari vya mtii?”.
Watakatifu wa siku
- Wenye Haki Yoakimu na Ana, wazazi wa Mama wa Mungu
- Mfiadini Severiani (320)
- Mtakatifu Mtawa Yusufu, abati wa Volokolamsk, mtenda miujiza (1515)
- Kupatikana na kuhamishwa kwa masalia ya Askofu Mtakatifu Theodosio, Askofu Mkuu wa Chernihiv (1896)
- Wafiadini wa Kikasisi Gregori, padri, na Aleksanda, shemasi (1918)
- Wafiadini wa Kikasisi Zakaria, Askofu Mkuu wa Voronezh, Basili, Sergio, Yusufu, Aleksi, mapadri, Demetrio, shemasi, na Mfiadini Basili (1937)
- Mtawa Mfiadini Androniko (1938)
- Mfiadini wa Kikasisi Aleksanda, padri (1942)
- Wafiadini Haritoni na Stratori (Stratoniko) (karne ya 3)
- Mtakatifu Mtawa Theofani Mwungamaji (karibu 300)
- Kumbukumbu ya Mtaguso wa Tatu wa Kiekumene (431)
- Mbarikiwa Niketa wa Konstantinopoli (karne ya 12)
- Mtakatifu Mtawa Onufrio wa Voronsk (1789)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 9 Septemba katika kalenda ya kanisa ni 22 Septemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki