Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Julai 2027 › 27 Julai

Kalenda ya Kiorthodoksi · 14 Julai (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 27 Julai 2027

Jumanne · Wiki ya 6 baada ya Pentekoste · Sauti ya 4

Sikukuu na watakatifu

Mtume Akila, wa Mitume 70 (karne ya 1)

Mfungo

Hakuna mfungo

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Waraka

1 Kor 1:1–9

1Paulo, aliyeitwa na Kristo Yesu kuwa mtume kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu, 2kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, kwa wale ambao wamewekwa wakfu katika Yesu Kristo, ambao wameitwa kuwa watu watakatifu. Tunawaandikia pia wale wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo katika mahali pote, Bwana wao na wetu. 3Neema na amani iwe kwenu kutoka kwa Mungu baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo. 4Siku zote namshukru Mungu wangu kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu ambayo Kristo Yesu aliwapa. 5Amewafanya kuwa matajiri katika kila njia, katika usemi na pamoja maarifa yote. 6Amewafanya matajiri, kama ushuhuda kuhusu Kristo ya kwamba amethibitishwa kuwa kweli miongoni mwenu. 7Kwa hiyo hampungukiwi karama za kiroho, kama mlivyo na hamu ya kusubiri ufunuo wa Bwana wetu Yesu Kristo. 8Atawaimarisha ninyi pia hadi mwisho, ili msilaumiwe siku ya Bwana wetu Yesu Kristo. 9Mungu ni mwaminifu ambaye aliwaita ninyi katika ushirika wa mwana wake, Yesu Kristo Bwana wetu.

Waraka (ya Jumatano)

1 Kor 2:9–3:8

9Lakini kama ilivyoandikwa, “Mambo mbayo hakuna jicho limeyaona, hakuna sikio lililoyasikia, mawazo hayakufikiri, mambo ambayo Mungu ameyaandaa kwa ajili ya wale wampendao yeye.” 10Haya ni mambo ambayo Mungu ameyafunua kwetu kupitia Roho, Kwa kuwa Roho huchunguza kila kitu, hata mambo ya ndani ya Mungu. 11Kwa kuwa nani afahamuye mawazo ya mtu, isipokuwa roho ya mtu ndani yake? Hivyo pia, hakuna ajuaye mambo ya ndani ya Mungu, isipokuwa Roho wa Mungu. 12Lakini hatukupokea roho ya dunia, lakini Roho ambaye anatoka kwa Mungu, ili kwamba tuweze kujua kwa uhuru mambo tuliyopewa na Mungu. 13Tunasema mambo haya kwa maneno, ambayo hekima ya mtu haiwezi kufundisha, lakini ambayo Roho hutufundisha. Roho hutafasiri maneno ya kiroho kwa hekima ya kiroho. 14Mtu asiye wa kiroho hapokei mambo ambayo ni ya Roho wa Mungu, kwa kuwa hayo ni upuuzi kwake. Hawezi kuyajua kwa sababu yanatambuliwa kiroho. 15Kwa yule wa kiroho huhukumu mambo yote. Lakini huhukumiwa na wengine. 16“Ni nani anaweza kuyajua mawazo ya Bwana, ambaye anaweza kumfundisha yeye?” Lakini tuna mawazo ya Kristo. 3:1Na mimi, kaka na dada zangu, sikusema nanyi kama watu kiroho, lakini kama na watu wa kimwili. Kama na watoto wadogo katika Kristo. 2Niliwanywesha maziwa na si nyama, kwa kuwa hamkuwa tayari kwa kula nyama. Na hata sasa hamjawa tayari. 3Kwa kuwa ninyi bado ni wa mwilini. Kwa kuwa wivu na majivuno yanaonekana miongoni mwenu. Je, hamuishi kulingana na mwili, na je, hamtembei kama kawaida ya kibinadamu? 4Kwa kuwa mmoja husema, “Namfuata Paulo” Mwingine husema “Namfuata Apolo,” hamuishi kama wanadamu? 5Apolo ni nani? na Paulo ni nani? Watumishi wa yule mliyemwamini, kwa kila ambaye Bwana alimpa jukumu. 6Mimi nilipanda, Apolo akatia maji, lakini Mungu akakuza. 7Kwa hiyo, si aliye panda wala aliyetia maji ana chochote. Lakini ni Mungu anayekuza. 8Sasa apandaye na atiaye maji wote ni sawa, na kila mmoja atapokea ujira wake kulingana na kazi yake.

Injili

Mt 13:24–30

24Yesu aliwapa mfano mwingine. Akisema, “Ufalme wa mbinguni unafananishwa na mtu aliye panda mbengu nzuri katika shamba lake 25Lakini watu waliposinzia, adui wake akaja pia akapanda magugu katikati ya ngano kisha akaenda zake. 26Baadaye ngano ilipoota na kutoa mazao yake, ndipo magugu yalitokea pia. 27Na watumishi wa mwenye shamba walikuja wakamwambia, 'Bwana, hukupanda mbengu nzuri katika shamba lako? Imekuwaje sasa lina magugu? 28Akawaambia, Adui ametenda hili.' Watumishi walimwambia, “Kwa hiyo unataka twende tukayang'oe?” 29Mwenye shamba akisema, 'Hapana, wakati mnayang'oa magugu mtang'oa pamoja na ngano. 30Yaacheni yakue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati wa mavuno nitasema kwa wavunaji, 'Kwanza yang'oeri magugu na yafungeni matita matita na kuyachoma, lakini kusanyeni ngano katika ghala langu.''''

Injili (ya Jumatano)

Mt 13:31–36

31Kisha Yesu aliwatolea mfano mwingine. Akasema, “Ufalme wa mbinguni unafanana na mbegu ya haradali ambayo mtu aliichukua na kuipanda katika shamba lake. 32Mbegu hii kwa hakika ni ndogo kuliko mbegu zingine zote. Lakini imeapo huwa kubwa kuliko mimea yote ya bustani, huwa mti, kiasi kwamba ndege wa angani huja na kujenga viota katika matawi yake.” 33Akawaambia mfano mwingine tena.”Ufalme wa mbinguni ni kama chachu ile iliyo twaliwa na mwanamke na kuichanganya kwa vipimo vitatu kwa unga mpaka viumuke. 34Hayo yote Yesu aliyasema kwenye umati kwa mifano. Na pasipo mifano hakusema chochote kwao. 35Hii ilikuwa kwamba kile kilichokwisha semwa kupitia kwa nabii kiweze kutimia, pale aliposema, “Nitafumbua kinywa changu katika mifano. Nitasema mambo yale yaliyokuwa yamefichwa tangu misingi ya ulimwengu”. 36Kisha Yesu aliwaacha makutano na kwenda nyumbani. Wanafunzi wake walimwendea na kusema, “Tufafanulie mfano wa magugu ya shambani.''

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 27 Julai

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 14 Julai katika kalenda ya kanisa ni 27 Julai katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki