Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Julai 2027 › 23 Julai

Kalenda ya Kiorthodoksi · 10 Julai (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 23 Julai 2027

Ijumaa · Wiki ya 5 baada ya Pentekoste · Sauti ya 3

Sikukuu na watakatifu

Wafiadini 45 wa Nikopoli ya Armenia: Leontio, Mauriki, Danieli, Antoni, Aleksanda, Ianikita, Sisinio, Menea, Virilado na wengine (karibu 319)

Siku ya mfungo

Mfungo: pamoja na mafuta

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Sala ya Jioni: somo

Haimo katika tafsiri hii

Sala ya Jioni: somo

Haimo katika tafsiri hii

Sala ya Jioni: somo

Haimo katika tafsiri hii

Sala ya Alfajiri: Injili

Mt 11:27–30

27Mambo yote yamekabidhiwa kwangu kutoka kwa Baba. Na hakuna amjuaye Mwana isipokuwa Baba, na hakuna amjuaye Baba isipokuwa Mwana, na yeyote ambaye Mwana ana hamu ya kumfunulia. 28Njoni kwangu, nyinyi nyote mnaosumbuka na mnaolemewa na mzigo mzito, nami nitawapumzisha. 29Jitieni nira yangu na mjifunze kutoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mnyenyekevu na mpole wa moyo na mtapata pumziko la nafsi zenu. 30Kwa kuwa nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.

Waraka

Rum 16:1–16

1Namkabidhi kwenu Fibi dada yetu, ambaye ni mtumishi wa kanisa ambalo liko Kenkrea, 2ili kwamba mnaweza kumpokea katika Bwana. Fanyeni hivi katika kicho cha thamani cha waumini, na msimame pamoja naye katika jambo lolote atakalokuwa na uhitaji nalo. Maana yeye mwenyewe amekuwa mhudumu wa wengi, na kwa ajili yangu mwenyewe. 3Msalimu Priska na Akila, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu, 4ambao kwa maisha yangu waliyahatarisha maisha yao wenyewe. Ninatoa shukrani kwao, na siyo tu mimi, bali pia kwa makanisa yote ya mataifa. 5Lisalimie kanisa ambalo liko nyumbani kwao. Msalimie Epanieto mpendwa wangu, ambaye ni mzaliwa wa kwanza wa Kristo katika Asia. 6Msalimie Mariamu ambaye ametenda kazi kwa bidii kwa ajili yenu. 7Msalimie Androniko na Yunia, jamaa zangu, na wafungwa pamoja nami. Ni wa muhimu miongoni mwa mitume, ambao pia walitangulia kumjua Kristo kabla yangu. 8Msalimie Ampliato, mpendwa wangu katika Bwana. 9Msalimie Urbano, mtenda kazi pamoja nami katika Kristo, na Stakisi mpendwa wangu. 10Msalimie Apele, mwenye kukubaliwa katika Kristo. Wasalimie wote ambao walio katika nyumba ya Aristobulo. 11Nisalimie Herodioni, jamaa yangu. Nisalimie wote walio katika nyumba ya Narkiso, ambao wako katika Bwana. 12Nisalimie Trifaina na Trifosa, wanaotenda kazi kwa bidii katika Bwana. msalimie Persisi mpendwa, ambaye ametenda kazi zaidi kwa Bwana, 13Nisalimie Rufo, aliyechaguliwa katika Bwana na mama yake na wangu. 14Msalimie Asinkrito, Flegon, Herme, Patroba, Herma, na ndugu wote walio pamoja nao. 15Nisalimie Filologo naYulia, Nerea na dada yake, na Olimpa, na waumini wote walio pamoja nao. 16Nisalimie kila mmoja kwa busu takatifu. Makanisa yote katika Kristo yawasalimu.

Waraka (Mt. Antoni)

Gal 5:22–6:2

22Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, ukarimu, utu wema, imani, 23upole, na kiasi. Hakuna sheria dhidi ya mambo kama hayo. 24Wale walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na shauku na tamaa zao mbaya. 25Kama tukiishi kwa Roho, pia tutembee kwa Roho. 26Tusiwe wa kujivuna, tusichokozane kila mmoja na mwenzake, wala tusioneane wivu. 6:1Ndugu, ikiwa mtu amekamatwa katika uovu, ninyi mlio wa kiroho, mnawiwa kumrejesha huyo ndugu katika roho ya upole. Huku mkijiangalia wenyewe ili msijaribiwe. 2Mchukuliane mizigo, na kwa hiyo mtaikamilisha sheria ya Kristo.

Injili

Mt 13:3–9

3Kisha Yesu alisema maneno mengi kwa mifano, Alisema, “Tazama, mpanzi alienda kupanda. 4Alipokuwa akipanda baadhi ya mbegu zilianguka kando ya njia na ndege walikuja wakazidonoa. 5Mbegu zingine zilianguka juu ya mwamba, ambapo hazikupata udongo wa kutosha. Ghafla zilichipuka kwa sababu udongo haukuwa na kina. 6Lakini jua lilipo chomoza zilichomwa kwa sababu hazikuwa na mizizi, na zilikauka. 7Mbengu zingine zilianguka kati ya miti yenye miiba. Miti yenye miiba ilirefuka juu ikaisonga. 8Mbegu zingine zilianguka kwenye udongo mzuri na kuzaa mbegu, zingine mara mia moja zaidi, zingine sitini na zingine thelathini 9Aliye na masikio na asikie.

Injili (Mt. Antoni)

Mt 4:25–5:12

25Umati mkubwa wa watu ulimfuata kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu na Uyahuda na kutoka ng'ambo ya Yorodani. 5:1Yesu alipo uona umati, akaondoka na kuelekea Mlimani. Alipokuwa ameketi chini, wanafunzi wake wakaja kwake. 2Akafunua kinywa chake na akawafundisha, akisema, 3“Heri walio maskini wa roho maana ufalme wa mbinguni ni wao. 4Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa. 5Heri wenye upole, maana watairithi nchi. 6Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watashibishwa. 7Heri wenye rehema maana hao watapata Rehema. 8Heri wenye moyo safi maana watamwona Mungu. 9Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu. 10Heri wale wanaoteswa kwa ajili ya haki, maana ufalme wa mbinguni ni wao. 11Heri ninyi ambao watu watawatukana na kuwatesa, au kusema kila aina ya ubaya dhidi yenu kwa uongo kwa ajili yangu. 12Furahini na kushangilia, maana thawabu yenu ni kubwa juu mbinguni. Kwa kuwa hivi ndivyo watu walivyo watesa manabii walioishi kabla yenu.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 23 Julai

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 10 Julai katika kalenda ya kanisa ni 23 Julai katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki