Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Julai 2027 › 3 Julai

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 3 Julai 2027

Jumamosi · Juma la 13 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Mt. Tomaso, mtume

Sikukuu · Rangi ya liturujia: nyekundu

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Efe 2:19–22

19Hivyo basi, ninyi watu wa mataifa si wasafiri na wageni tena. Bali ni wenyeji pamoja na wale waliotengwa kwa ajili ya Mungu na wajumbe katika nyumba ya Mungu. 20Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii. Kristo Yesu mwenyewe alikuwa jiwe kuu la pembeni. 21Katika yeye jengo lote limeungamanishwa pamoja na kukua kama hekalu ndani ya Bwana. 22Ni ndani yake ninyi nanyi mnajengwa pamoja kama mahali pa kuishi pa Mungu katika Roho.

Wimbo wa katikati

Zab 117:1–2

1Msifuni Yahwe, enyi mataifa yote; enyi watu mhimidini yeye. 2Kwa kuwa uaminifu wa agano lake ni mkuu kwetu, na uaminifu wa Yahwe wadumu milele. Msifuni Yahwe.

Injili

Yn 20:24–29

24Thomaso, mmoja wa wale kumi na wawili, aliyeitwa Didimas, hakuwa na wanafunzi wenzake Yesu alipokuja. 25Wale wanafunzi wengine waka mwambia baadaye, “Tumemwona Bwana.” Naye akawambia, “Kama sitaona alama za misumari katika mikono yake, na kuweka vidole vyangu kwenye hizo alama, na pia kuweka mkono wangu kwenye ubavu wake sitaamini.” 26Baada ya siku nane wanafunzi walikuwa chumbani tena, naye Thomaso alikuwa pamoja nao. Wakati milango ilipokuwa imefungwa Yesu alisimama katikati yao. na akasema, “Amani na iwe nanyi.” 27Kisha akamwambia Thomaso, leta kidole chako na uone mikono yangu; leta hapa mikono yako na uweke kwenye ubavu wangu; wala usiwe asiyeamini bali aaminiye.” 28Naye Thomaso akajibu na kumwambia, “Bwana wangu na Mungu wangu.” 29Yesu akamwambia, Kwa kuwa umeniona, umeamini. Wamebarikiwa wao wanaoamini, pasipokuona.”

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 3 Julai

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki