Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Juni 2027 › 22 Juni

Kalenda ya Kiorthodoksi · 9 Juni (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 22 Juni 2027

Jumanne · Wiki ya 1 baada ya Pentekoste · Sauti ya 7

Sikukuu na watakatifu

Siku ya Tatu ya Utatu

Wiki isiyo na mfungo

Hakuna mfungo

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Waraka

Rum 1:1–7, 13–17

1Paulo, mtumishi wa Yesu Kristo, aliyeitwa kuwa mtume, na kutengwa kwa ajili ya Injili ya Mungu. 2Hii ndio ile Injili aliyoiahidi zamani kupitia manabii wake katika maandiko matakatifu. 3Ni kuhusu Mwana wake, aliyezaliwa kutoka ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili. 4Yeye alitangazwa kwa Mwana wa Mungu kwa nguvu ya Roho ya utakatifu kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo Bwana wetu. 5Kupitia yeye tumepokea neema na utume kwa utii wa imani kati ya mataifa yote, kwa ajili ya jina lake. 6Kati ya mataifa haya, ninyi pia mmeitwa kuwa wa Yesu Kristo. 7Barua hii ni kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watu watakatifu. Neema na iwe kwenu, na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo. 13Sasa ndugu, sitaki mkose kufahamu kwamba, mara nyingi nimekusudia kuja kwenu, lakini nimezuiliwa mpaka sasa. Nilitaka hivi ili kuwa na matunda kwenu kama ilivyo pia miongoni mwa watu wa mataifa. 14Nadaiwa na Wayunani na wageni pia, werevu na wajinga. 15Kwa hiyo, kwa upande wangu, mimi niko tayari kutangaza injili kwenu pia ninyi mlio huko Roma. 16Kwa maana siionei haya injili, kwa kuwa ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza na kwa Myunani pia. 17Kwa maana haki ya Mungu imedhihirishwa kutoka imani hata imani, kama ilivyo andikwa, “Mwenye haki ataishi kwa imani.”

Injili

Mt 4:25–5:13

25Umati mkubwa wa watu ulimfuata kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu na Uyahuda na kutoka ng'ambo ya Yorodani. 5:1Yesu alipo uona umati, akaondoka na kuelekea Mlimani. Alipokuwa ameketi chini, wanafunzi wake wakaja kwake. 2Akafunua kinywa chake na akawafundisha, akisema, 3“Heri walio maskini wa roho maana ufalme wa mbinguni ni wao. 4Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa. 5Heri wenye upole, maana watairithi nchi. 6Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watashibishwa. 7Heri wenye rehema maana hao watapata Rehema. 8Heri wenye moyo safi maana watamwona Mungu. 9Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu. 10Heri wale wanaoteswa kwa ajili ya haki, maana ufalme wa mbinguni ni wao. 11Heri ninyi ambao watu watawatukana na kuwatesa, au kusema kila aina ya ubaya dhidi yenu kwa uongo kwa ajili yangu. 12Furahini na kushangilia, maana thawabu yenu ni kubwa juu mbinguni. Kwa kuwa hivi ndivyo watu walivyo watesa manabii walioishi kabla yenu. 13Ninyi ni chumvi ya dunia. Lakini kama chumvi imepoteza ladha yake, itawezaje kufanyika chumvi halisi tena? Kamwe haiwezi kuwa nzuri kwa kitu kingine chochote tena, isipokuwa ni kutupwa nje na kukanyagwa na miguu ya watu.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 22 Juni

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 9 Juni katika kalenda ya kanisa ni 22 Juni katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki